Wednesday, March 20, 2019 Home|Habari|فارسي|Kiswahili
 

Nyumbani|Uislamu|Lugha ya Kifursi|FAQ|Wasiliana nasi|Links|Sitemap
Title
iran
.
Login
Username :   
Password :   
 
Captcha:
[Signup]
NewsletterSignup
Name :   
E-mail :   


  Print        Send to Friend

Kumbukumbu ya 33 ya Ushindi ya Mapinduzi ya Iran

Februari 11 ni siku ya ushindi wa ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu na ni siku ya kitaifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Mapinduzi haya kihistoria katika taifa la Iran linalojidhihirisha kama Mapinduzi ya Kiislamu, vuguvugu lililoashiria utashi wa taifa wa kuweka mamlaka yake na kuamua njia yake. Ushindi wa mapinduzi matukufu ya Kiislamu mnamo februari 1, 1979, ulioletwa na uongozi wa Imam Khomeini (Allah amlipe pepo), na uliokuwa na malengo mapana yaliyosheheni misingi ya haki za kibinadamu pamoja na maadili ya Kiislamu, ni mafanikio makubwa katika mchakato wa mapinduzi, ambayo, kwa hakika yalianza mwaka 1963. Mwezi wa Moharram wa mwaka 1963 ulipoingia, maulamaa wakaanza kutoa hotuba za kisiasa na maadhimisho ya msiba, kumbukumbu ya kifo cha Imam Husein (a.s) aliyekuwa ni mjukuu mtukufu wa mtume (s.a.w.w) na Imam wa tatu wa nyumba ya Mtukufu Mtume Muhammad ( s.a.w.w) maadhimisho hayo yakageuka kuwa majukwaa ya kisiasa kwa ajili ya kuukosoa utawala huo. Jioni ya Ashura (siku ambayo Imam Hussein na wafuasi 72 waliuwawa na kufa wakawa ni mashahidi) Imam Khomeini alitoa hotuba katika chuo cha theolojia cha Feizieh ambapo idadi kubwa ya watu ilikuwa imekusanyika, akimkosoa Shah, mauaji na uvunjaji wa sheria. Vilevile alielezea tishio la Israeli na hamasisho linaloutishia uislamu na raia. Akimweleza Shah, Imam Khomeini alisema “Ewe mheshimiwa mfalme, ninakushauri kuacha kuchukua hatua hizi”. Juni 4, 1963 (Moharram 11 Imam Khomieni alitiwa nguvuni katika mji wa Qom akapelekwa Tehran ambapo alifungwa. Watu walipopata habari ya kukamatwa kwa Imam Khomeini siku iliyofuata walifanya maandamano makubwa katika miji mikubwa kama vile Tehran, Qom, Shirazi, Mashhadi n.k. Serikali ilijibu mapigo kwa nguvu na mamia ya watu walitiwa nguvuni na wengine wengi wakajeruhiwa. Mnamo Machi 7, 1963, waziri mkuu Assadullah Alam alijiuzulu na Hassaali Mansour akashika nafasi yake. Baada ya miezi kadhaa ya kuwa kizuizini mjini Tehran Imam Khomeini aliachiwa huru tarehe 6, April, 1964 na akapelekwa Qom wakati wa usiku. Kutokana na Imam kurejea Qom, sherehe ya makaribisho ilifanyika katika shule ya theolojia ya Feizieh na azimio la vipengele 10 lilitolewa na wanafunzi wa theolojia. Azimio hilo lilijumuisha vipengele vifuatavyo:- 1. kutengeneza nidhamu kamili na kuandaa mipango ya kimsingi katika vituo vya kieleimu hasa katika seminari ya Qom. 2. Utekelezaji wa katiba katika maana yake ya kweli, hasa kipengele cha 2 na nyongeza yake. 3. utekelezaji sahihi wa sheria ya kiislamu na uhuishaji wa desturi za kidini zilizotelekezwa. 4. kutengua sheria na miswada inayopinga dini na kukomesha mabunge yote mawili ambayo si halali. 5. kukata mawasiliano ya mawakala wa kikoloni na utawala wa kizayuni nchini. 6. kukomesha dhulma na ufisadi. kueneza uadilifu wa kijamii, kukidhi mahitaji ya wananchi na kuunda Iran inayojitegemea, iliyohuru nchini ya bendera ya madhhabi ya Jaafari. 7. kuboresha mazingira ya kiuchumi, kuinua hali ya wafanyakazi na kutengeneza fursa za kazi kwa wahitimu. 8. kuzuia uasherati na program za sinema zilizo kinyume na maadili,n.k 9. kuwaacha huru wafungwa wote wasiokuwa na hatia, hasa Hujatul islam Seyed Mahmoud Taleqani, maprofesa wa chuo kikuu na kuwarejesha nyumbani wananchi waliopelekwa uhamishoni. 10. kuziangalia familia za mashahidi wa tukio la Juni 3. Mnamo Oktoba 12,1964, bunge lilipitisha mswada wa sheria kuhusu kinga ya washauri wa kimarekani waliopo nchini Iran, iliyoitwa “ sheria ya kusalimu amri”, mnamo Oktoba 25,1964, Imam Khomeini alitoa hotuba katika msikiti mkuu wa Qom ambapo aliikosoa vikali sheria hiyo na kuielezea kuwa ni mhimili wa kuwaweka Wairan utumwani na kuvunja uhuru wa nchi. Vilevile alimkaripia Shah akisema; kama nchi yetu iko chini ya uvamizi wa Marekani kwa nini hutangazi. Utawala wa Shah ulipompeleka Imam Khomeini uhamishoni nchini Uturuki hapo Novemba 3, 1964 mawimbi ya upinzani yaliunguruma miongoni mwa maulamaa wa kidini na watetezi wa harakati za kiislam. Maandamano ya wananchi yalifanyika Tehran, Qom na baadhi ya miji mingine, lakini utawala huo uliendeleza ukandamizaji dhidi ya raia. Mtoto mkubwa wa Imam, Seyed Mostafa Khomeini naye pia alitiwa nguvuni na kisha kupelekwa uhamishoni nchini Uturuki. Kufuatia makubaliano baina ya serikali za Uturuki na Iran, Imam Khomeini na mwanawe walipelekwa Najaf, Iraq, mnamo Oktoba 3, 1965. Machi 1, 1965 mfalme Shah alimtangaza mkewe Farah Diba, kuwa malkia wake, kwa kuwa uamuzi huo ulikuwa kinyume na katiba. Serikali ilitangaza kuwa sehemu ya bunge ingeitishwa mnamo April ili kuifanyia mabadiliko katiba. Wanafunzi wa kidini walitangaza upinzani wao dhidi ya uamuzi huo. Imam Khomeini alitangaza kuanzia sasa na kuendelea lengo la harakati litakuwa ni kumuondosha Shah na utawala wake. Sherehe za kumtawaza mfalme zilifanyika katika mwezi wa Oktoba mwaka 1967. Imam Khomeini alizishutumu sherehe hizo. Februari 1969 Imam Khomeini alianza kutoa mfululizo wa mihadhara kuhusu uongozi wa mwanafiqhi (Welayat Faqih). Baadaye mihadhara yake ilikusanywa katika muundo wa kitabu kilichoitwa “Welayat Faqih”, ambacho kilichapishwa Iran na katika nchi kadhaa za kiarabu. Utawala huo ulifanya sherehe katika mwaka 1971 kuuadhimisha mwaka wa 2500 wa ufalme nchini Iran. Makutano hayo yalihusisha anasa na ubadhirifu, jambo ambalo liliongeza ghadhabu na hasira za wananchi. Imam Khomeini pia alilaani sherehe hizi. Miaka ya 1971 mpaka 1975 iliashiria mwisho wa kamatakamata, mateso na ukandamizwaji wa wanaharakati uliokuwa ukifanywa na utawala huo. Bei za mafuta zilipopanda ghafla mwaka 1973, Shah alitangaza mpango wenye lengo endelevu ulioitwa kama ustaarabu mkubwa. Shah alitangaza kuanzisha chama cha Rastakhiz (baath) mnamo Machi 1 1974, kama chama pekee cha kitaifa chenye misingi mitatu ya kanuni. Katiba, ufalme na mapinduzi meupe. Imam Khomeini alitangaza kuwa uanachama wa chama hicho haukuwa halali na akakigomea chama. Uamuzi wa serikali katika 1976 wa kubadili kalenda ya Kiiran ambayo ilikuwa imesimama kwenye tukio la Hijra ya Mtume Muhammad kutoka Makka kwenda Madina na kuifanya kuwa kalenda ya kifalme inayosimamia kwenye uanzishwaji wa ufalme nchini Iran uliofanywa na Achaemenid Dynasty mwaka 55 BC, jambo hilo liliwaudhi maulamaa wa kidini halikadhalika wanaharakati wa kisiasa. Jimmy Carter, mgombea wa chama cha democtratic alipochaguliwa kuwa rais wa Marekani mwaka 1976 aliwataka marafiki zake ikiwemo Iran kuheshimu haki za kibinadamu. Hivyo Shah alifungua mazingira ya kisiasa ambayo yalitoa uwanja kamili kwa uenezaji wa Mapinduzi. Ayatollah Seyed Mostafa Khomeini, motto mkubwa wa Imam Khomeini, aliuawa na mawakala wa utawala wa Shah mjini Najaf mnamo Oktoba 22, 1977. Habari za kifo chake ziliongeza damu mpya katika vuguvugu la Wairan. Imam Khomeini alitoa hotuba akiwa katika makazi yake mjini Najaf mnamo Oktoba 31, 1977 na kaseti za hotuba yake zilisambazwa nchini Iran na taifa la Iran iliichukulia hotuba hiyo kama muongozo kwa ajili ya kukusanya nguvu za kufanya harakati dhidi ya utawala. Gazeti la kila siku la Kifarsi liitwalo Ittila’at lilichapisha makala mnamo Januari 6, 1978 iliyoitwa “Iran na ukoloni mweusi na mwekundu” makala hiyo iliandikwa na mtu aliyejiita Ahmad Rashid Motlaq ambapo ilimkashifu Imam Khomeini. Wanafunzi wa kitheolojia pamoja na kundi kubwa la wananchi walimiminika katika mitaa ya Qom mnamo Januari 8, 1978 katika maandamano dhidi ya makala hayo lakini utawala uliwashambulia ukaua idadi kadhaa ya waandamanaji. Kufuatia tukio hilo katika mji wa Qom Imam Khomeini katika maelezo yaliyoitwa “kipindi cha utawala kandamizi na haram wa Shah” alisema; “Carter na wanyonyaji wengine wa mali ya wanyonge wanatakiwa kutambua kuwa Muhammad Reza ni msaliti na iliyotengwa na jamii na ataondolewa madarakani”. Marajii wakubwa wa kidini waliwataka watu waadhimishe kumbukumbu ya siku ya 40 ya vifo vya watu waliouwawa katika mji wa Qom. Taifa la Iran ilifanya maadhimisho nchini kote kwa heshima ya mashahidi. Polisi walifanya mashambulizi kwenye maadhimisho yaliyofanyika mjiniTabrizi mnamo Februari 17, 1978 na kuua idadi kadhaa ya washiriki. Sherehe za mwaka mpya wa 1978 (Nowrouz) zilitangazwa kama msiba wa kitaifa. Kumbukumbu ya Juni 4, 1962 (mashambulizi kwenye chuo cha theolojia cha Feizieh) zilifanyika mwaka 1978 kwa kufunga maduka. Kutokana na maelekezo ya Imam Khomeini katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka) 1978 maulamaa wa kidini waligeuza mikutano yao ya kidini na kuwa vipindi vya kisiasa, mapinduzi kwa kuushambulia utawala wa wakala wa upelelezi wa Shah (Taasisi ya Taifa ya Usalama na Upelelelezi-SAVAK) walishambulia ukumbi wa sinema huko Abadan mnamo Agosti 18, 1978 ambapo zaidi ya watu 400 waliunguzwa mpaka wakafa. Kitendo hiki cha kutisha kiliwaghadhibisha watu, hasa wakazi wa mkoa wa Khozestan. Kufuatia kujiuzulu kwa waziri mkuu Jamshid Amuzagar hapo Agosti 26, 1978, Jaafar Sharif Imamii alitakiwa kuunda baraza la mawaziri. Alilitambulisha baraza lake hilo kuwa ni “serikali ya Umoja wa Kitaifa”. Ili kujionyesha kuwa ni mwanadini, Sharif Imamii alisema kuwa alikuwa mfuasi wa Ayatollah Kazem Shariatmadri. Alibatilisha kalenda ya kifalme, akapiga marufuku kasino, akatoa uhuru kwa vyombo vya habari, aliahidi kuwaadhibu wale wanaohusika na ufisadi wa mali, kuwaachia huru wafungwa wa kisiasa, kupunguza kodi na kukivunja chama cha Rastahriz . Sala ya jamaa ya aina yake iliyoongozwa na Ayatolah Mofateh ilifanyika mnamo Septemba 2, 1978 katika eneo la Qeitariyeh-mjini Tehran. Ilionyesha mshikamano na uimara wa watu dhidi ya udikteta. Radio ya nchi ilitangaza muda wa kuzima taa, moto na kufunga milango katika mji wa Tehran na miji mingine mikubwa 12 mnamo asubuhi ya tarehe 7 Septemba. Lakini watu hao bila ya kujua hali iliyotangazwa, walikusanyika katika uwanja wa mashahidi wa Tehran na hawakuondoka hapo hata baada ya jeshi kuwaamuru watawanyike. Wanajeshi hao walianza kuwatupia risasi watu hao kwa masaa kadhaa na kusababisha msiba mkubwa.tukio hilo lilijulikana kama “Ijumaa nyeusi”. Mwaka wa masomo ulipoanza, ushiriki wa wanafunzi wa chuo Kikuu na wale wa elimu ya juu uliongezeka zaidi. Walimchukulia Imam kuwa ndiye nguzo muhimu kwa maendeleo yote, hivyo utawala wa Shah ulifikiria kufanya baadhi ya maandalizi ili kumhamisha Imam Khomeini kutoka Iraq. Kutokana na ushauri wa utawala wa Shah, utawala wa Iraq ulimtaka Imam Khomeini akae kimya au aondoke Iraq. Imam Khomeini alihiyari chaguo la pili na hivyo kuelekea Kuwait. Lakini Kuwait haikumpa viza ya kuingia, mnamo Septemba 4 , 1978 Imam Khomeini alielekea Ufaransa na kuishi katika eneo la Naufle de chateau. Kinyume na mawazo ya Shah, kuhama kwa Imam kwenda Ufaransa kuliongeza damu mpya katika mwili wa harakati. Migomo ya wafanyakazi wa kiwanda cha mafuta, kampuni ya mawasiliano, benki ya taifa, idara ya ugavi wa maji, taasisi ya barabara na usafirishaji, redio na televisheni, na ofisi nyingine za umma mnamo Oktoba ilipanua wigo wa harakati. Migomo hiyo ilipoozesha mfumo wa utawala wa umma. Mnamo Oktoba 26, 1978 kwa msaada wa serikali na jeshi, Ardeshir Zahedi aliandaa maandamano mjini Tehran katika kuunga mkono katiba. Meja Jenerali Gholamreza Azhari alitakiwa kuunda baraza la mawaziri mnamo Novemba 4, 1978. Katika ujumbe wa televisheni Shah aliwataka wanasiasa na viongozi wa kidini kuisaidia serikali kubadilisha mambo na akasema kuwa amesikia ujumbe wa mapinduzi wa taifa la Iran. Pia alisema; sheria za kijeshi ni za mpito chaguzi zitafanyika baada ya amani na usalama kudhibitiwa, wala rushwa wataadhibiwa, katiba itatekelezwa na makosa yaliyopita yatafidiwa. Mwanzoni serikali ya Azhari ilichukua udhibiti wa vyombo vya habari, lakini waandishi wa habari walifanya mgomo na waliendeleza migomo yao mpaka serikali ya Azhari ikaanguka. Maandamano makubwa yalifanyika katika siku za Ta’sua na Ashura ya mwaka 1978 yalikuwa ni kama kura ya maoni kwa ajili ya Jamhuri ya kiislamu na kulikomesha utawala wa kifalme. Azimio la nukta 17 lilikuwa na nukta zifuatazo kama malengo na vuguvugu la kimapinduzi la taifa la Iran, kumuondosha Shah madrakani, kuutambua uongozi wa Imam Khomeini, kuanzisha serikali ya Kiislam kulinda haki za binadamu, kulinda haki za kisiasa za raia wote kulinda haki za wafanyakazi na wakulima na kuweka uadilifu wa kijamii katika jamii. Azhari alipodhoofika Shah alimteua Shahpour Bakhtiyar, aliyekuwa mpiganaji wa jeshi la taifa kuwa waziri mkuu. Akitangaza “demokrasia ya kijamii” kama kauli mbiu yake, Bakhtiyar alishika usukani, pale generali Howzer, mjumbe maalum wa Carter alipokuja Iran kulibembeleza jeshi limuunge mkono Bakhtiyar vile vile Shah alijaribu kulinda taji lake kwa kuunda baraza la kifalme. Mnamo Januari 15, 1979, Mohammadreza Shah alilazimika kuondoka Iran, Imam akatangaza kuwa serikali ya Baktiyar haikuwa halali na akamuita kuwa ni msaliti na mkosefu. Wakati harakati za wananchi zikiendelea chini ya uongozi wa Imam Khomeini aliwapa muongozo muhimu ili kulinda mali ya taifa na kuzuia machafuko. Aliahidi kuunda “Baraza la Mapinduzi” mapema mno. Maandamano makubwa yalifanyika katika mji wa Tehran pamoja na miji mingine katika tukio la Arba’in (kumbukumbu ya siku ya 40 ya kifo cha Imam Hussein). Azimio la nukta kumi lilichapishwa na waandamanaji mjini Tehran wakiita serikali ya Bakhtiyar kuwa isiyokuwa halali na kumtaka Imam Khomeini kuunda baraza la mapinduzi mapema iwezekanavyo. Siku hiyo hiyo ilitangazwa kuwa Imam Khomeini angerejea Iran mapema. Bakhtiyar alifunga viwanja vyote vya ndege nchini. Katika radiamali yao wananchi walipanga kufanya maandamano zaidi nchi nzima. Hatimaye uwanja wa ndege wa Mehrabad wa mjini Tehran ulifunguliwa ambapo ndege iliyomchukua Imam Khomeini na kiongozi, wakiwa pamoja na idadi kadhaa ya wanaharakati waliopelekwa uhamishoni, iliwasili Tehran mnamo Januari 31, 1979. Imam Khomeini alielekea kwenye uwanja wa Mashahidi wa mapinduzi ambapo alitoa hotuba iliyotangaza kuwa serikali ya Bakhtiyar siyo halali na akaahidi kutangaza wanachama wa baraza la mapinduzi. Mnamo Februari 8, 1979 idadi kubwa ya watumishi wa jeshi la anga walikwenda nyumbani kwa Imam Khomeini na kula kiapo cha utii kwake. Mgongano ulizuka kati ya baadhi ya watumishi wa jeshi la anga na walinzi wa ufalme mnamo Februari 9. Wananchi walifanya haraka kuwasaidia wanajeshi wa jeshi la anga na hivyo milago ya kambi ya jeshi ikafunguliwa ambapo wananchi waliingia na kuchukua silaha kutoka kwenye ghala. Hatimaye wakuu wa vikosi vya majeshi walitangaza kutwaa serikali. Mnamo Februari 10 saa 10 jioni walitangaza muda wa kuzima taa na kufunga milango. Imam aliwataka watu wasitii agizo hilo. Watu waliendelea kukimbilia kwenye vituo vya kijeshi na polisi na wakaviteka huku wakikabiliana na upinzani mdogo. Mnamo Februari 11, 1979 mfumo wa ufalme wenye miaka 2500 pamoja na utawala wa Pahlavi uliodumu kwa miaka 50 ulianguka na ‘Jamhuri ya Kiislam ikaanzishwa’.


10:18 - 10/02/2012    /    Number : 577094    /    Show Count : 7245


Users Comment
No Comment for this news
Your Comment
Name :
E-mail : 
*Comments :
Captcha:
 

Search
Advance Search Web Search
banners
Kiongozi Muadhama

Imam

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

presstv

Radio Tehran

Al-hikma

Iqna

Irna

Mubaligh

Jamiatul Mustafa (SAWW

Islamica

Rayhanee
vote
Disable
UsersStats
Visitorsofpage: 27611
Visitorsofday : 20
Visitorsofpage : 70382
Onlinevisitors : 1
PageLoad : 1.2032

Home|Habari|Kutuhusu|Programu|Historia ya mahusiano ya kitamaduni|Mahusiano ya jumuia zingine |Machapisho|Ushirikiano na Maktaba zingine|Matukio ya Kiutamaduni|Ofisi zingine za Iran