Wednesday, March 20, 2019 Home|Habari|فارسي|Kiswahili
 

Nyumbani|Uislamu|Lugha ya Kifursi|FAQ|Wasiliana nasi|Links|Sitemap
Title
iran
.
Login
Username :   
Password :   
 
Captcha:
[Signup]
NewsletterSignup
Name :   
E-mail :   


  Print        Send to Friend

Maadhimisho ya Kifo cha Imam Khomeini (RA)

Siku ya Jumapili ya tarehe 3 mwezi wa sita mwaka 2012 kituo cha utamaduni cha Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kiliandaa semina ya kumbukumbu ya Muasisi wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. Semina hiyo ilifanyika katika ukumbu wa Ja’fari au zamani ulijulikana kama Ukumbi wa Korea. Semina ilianza muda wa saa nne asubuhi kwa kisomo cha Qur’ an tukufu iliyosomwa na Ustadhi Abdallah Rajab kutoka Magomeni Jijini Dar es Salaam. Baada ya kisomo cha Qur’ ani ililuwa zamu ya Mkurugenzi wa Kituo Bw. Morteza Sabouri kuwakaribisha wageni waalikwa katika semina, na akachukua nafasi ya kumualika rasmi mgeni rasmi mheshimiwa waziri wa sayansi bwana Mbarawa ili awasilishe mada aliyoindaa kwa ajili ya kutoa mchango wake. Awali ya yote napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kutuwezesha kufika hapa kwa aajili ya shuguli yetu hii adhimu, leo jamhuri ya Iran na waislamu wote duniani wanaadhimisha miaka 23 ya kumbukumbu ya kifo cha Imam Khomeini mwenyezi mungu amrehemu, katika kufanya hivyo lazima tujikumbushe mambo ambayo Imam Khomeini aliyapa kipaumbele cha juu, lakini kabla ya kufanya hivyo ni lazima kwanza tumjue imam Khomeini, Imam Khomeini,alizaliwa katika mji mdogo unaoitwa Khomeini uliopo nchini Iran mnamo tarehe 24,Septemba,1902. Alizaliwa katika familia ya wasomi ambao vizazi vyao viliyatoa maisha yao sadaka katika uongozi wa kidini ili kuwaongoza idadi kubwa ya watu wenye njaa ya maarifa. Ruhullah akiwa kijana,alianza elimu yake kwa kuhifadhi Quran Tukufu,na baadae alitumwa kwenda katika mji wa Arak mwaka (1920-1921), na hatimaye alitumwa kwenda mjini Qom mwaka (1923) ili kukamilisha masomo yake ya kidini.Mnamo miaka ya 1930s,Imam Khomeini hakuingia katika shughuli za kisiasa,badala yake alijitolea muda wake wote katika kufundisha Falsafa ya sheria ya Kiislaam katika mji wa Qom. Ndugu waalikwa mabibi na mabwana, Imam Khomeini aliyapa kipaumbele mambo yafuatayo La kwanza kabisa, jambo lakwanza ni kujenga taifa la wairan lenye umoja na mshikamano. Imam Khomeini alikuwa na matumaini makubwa kwamba si Iran tu bali mataifa yote ya Kiislamu yangejikwamua kutoka fikra potofu ya kutegemea mataifa mengine na kuzingatia utamaduni wao uliojaa utajiri mkubwa kutokana na mafundisho ya dini ya Kiislamu, kutokana na fikra zake za kimapinduzi Imam Khomeini alipanda na kupalilia mbegu ya kujitegemea na kujiamini katika mioyo ya wairan. Jambo lapili ambalo ni muhimu ambalo imam Khomeini aliamini katika maisha yake yote ni kama lifuatalo, jambo la pili ambalo alilipa kipa umbe ni usawa wa kibinadamu, kwnza ilikuwa ni kudumisha umoja wa kitaifa, ambalo kama sisi waumini wa dini ya kiislamu lazima tudumishe umoja wa kitaifa, hili lilikuwa ni kipaumbele kikubwa cha Imam khomeni, kipaumbele kingine ni kumisha misingi ya heshma kwa kila mtu na usawa wa kibinadamu, huu ni msingi ambao imam Khomeini alikuwa anaumini katika maisha yake yote, na kujenga jumuiya usawa kwa kila binadamu hayo ndo mambo ambayo imam Khomeini alikuwa anayapa kipaumbele katika maisha yate. Imam Khomeini aliendelea kuwa na mambo mengi sana ambyo kama nikiyataja yanaweza kutufikisha mpaka asubuhi laini nimeyachagua hayo mambo mawili ambayo imam Khomeini aliyagusia na sisi waislamu wote inabidi tuyatimize. Hayo yalikuwa hutuba ya Waziri Mbarawa Baada ya Waziri alifuatia Balozi wa Jamhri ya Kiislamu ya Iran Bw. Muvahid Ghommi ambaye naye kwa upande wake alieza wasifu wa Imam Khomeini na mafanikio yalopatikana Iran leo hii ni matunda mazuri aloweka Imam Khomein, Iran leo imepiga hatua kubwa sana katika Nyanja mbalimbali za kiuhumi na sayansi kwani Iran leo pamoja na kuwa katika vikwazo vya kiuchumi lakini imesimama imara sana. Baada ya Balozi aliuata Sheikh Alibasalehe ambaye alisisitiza namna ya kuwa waislamu inabidi wawe na maandalizi juu maadui zao kwa kusoma aya ya Qur ani iliyosema na muandaliye kwa kila muwezalo kutokana na nguvu ili muwatishe maadui zenu na maadui wa mwenyezi mungu Mwisho semina ilihitimishwa kwa dua kutoka kwa DKt Ahmad Khatib. Baada ya dua waumini walikusanyika kwa ajili ya Ibada ya sala ya Adhuhuri na baada ya sala walipata Tabaru yaani chakula cha mchana.


17:03 - 05/06/2012    /    Number : 583965    /    Show Count : 616


Users Comment
No Comment for this news
Your Comment
Name :
E-mail : 
*Comments :
Captcha:
 

Search
Advance Search Web Search
banners
Kiongozi Muadhama

Imam

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

presstv

Radio Tehran

Al-hikma

Iqna

Irna

Mubaligh

Jamiatul Mustafa (SAWW

Islamica

Rayhanee
vote
Disable
UsersStats
Visitorsofpage: 27610
Visitorsofday : 17
Visitorsofpage : 70379
Onlinevisitors : 1
PageLoad : 1.2187

Home|Habari|Kutuhusu|Programu|Historia ya mahusiano ya kitamaduni|Mahusiano ya jumuia zingine |Machapisho|Ushirikiano na Maktaba zingine|Matukio ya Kiutamaduni|Ofisi zingine za Iran