Saturday, March 23, 2019 Home|Habari|فارسي|Kiswahili
 

Nyumbani|Uislamu|Lugha ya Kifursi|FAQ|Wasiliana nasi|Links|Sitemap
Title
iran
.
Login
Username :   
Password :   
 
Captcha:
[Signup]
NewsletterSignup
Name :   
E-mail :   


  Print        Send to Friend

Kuzaliwa kwa Imam Mahdi

Imam Mahdi AS alizaliwa siku ya Ijumaa ya mwezi 15 Shaabani mwaka 255 Hijria mjini Samarra Iraq na baba yake akiwa ni Imam Hassan Askari AS. Imam Mahdi ni mjukumuu wa Bwana Mtume Muhammad SAW kupitia kizazi cha masharifu na masayyid cha binti mtukufu wa Bwana Mtume Muhammad yaani Bibi Fatimatu Zahra SA. Mama yake alikuwa Bibi mwenye heshima kubwa aliyejulikana na jina la Nargis. Imam Mahdi AS ni nyota ya 12 ya Maimamu wa Ahlul Bayt AS waliousiwa na Bwana Mtume Muhammad SAW. Ni vyema kusema pia hapa kwamba masuala mengi yanayohusiana na Imam Mahdi AS ni mambo ya ajabu ikiwa ni pamoja na namna ya kuzaliwa kwake kiasi kwamba hata athari za ujauzito wa mama yake haukuwa wa kawaida na wala hazikuonekana hadharani athari za ujauzito wake. Siri ya jambo hilo nayo iko wazi kwamba watawala wa wakati huo wa Bani Abbas walikuwa wamesoma hadhithi kutoka kwa Bwana Mtume Muhammad SAW na Maimamu watoharifu kuwa Imam Hassan Askari AS angelizaa mtoto ambaye angelikuja kuvunja tawala zote za kidhalimu na kidikteta, na kuangamiza kambi zote za upotofu na ufisadi na hatimaye kuijaza ardhi uadilifu na haki. Hivyo majasusi wa watawala wa Bani Abbas wakawa wanafuatilia kwa karibu sana maisha ya watu wa nyumbani kwa Imam Askari AS kwa nia ya kuzuia kuzaliwa mtoto huyo na kama wakiona amezaliwa, wamuue mara moja. Hivyo namna ya kuchukuliwa mimba, kuzaliwa na maisha ya baadaye ya Imam Mahdi AS hayakuwa na hali za kawaida. Kwa hakika Mwenyezi Mungu alitaka Imam Mahdi azaliwe katika mazingira yanayofanana na yale ya Nabii Musa AS. Maadui wa Imam Mahdi walitumia mbinu ile ile iliyotumiwa na majasusi wa Firauni waliofanya ujasusi na njama kubwa za kutaka kumuua Nabii Musa AS akiwa bado mdogo. Hata hivyo Mwenyezi Mungu kwa uwezo Wake alimuokoa Mtume Wake huyo. Watawala wa Bani Abbas nao walitaka kuzuia kuzaliwa Imam Mahdi AS na kumuua akiwa bado mchanga. Waliwawekea ulinzi mkali - mbali na majasusi wengi - watu wa nyumba ya Imam Askari AS, lakini Mwenyezi Mungu amemlinda Imam Mahdi AS hadi leo hii.

 

Baada ya kutimia uthibitisho wa kiimani juu ya uwelewa wa Mahdi kwa madhehebu ya Ahlul-Bait (a.s.) sasa tunaingia hatua mpya ya uchunguzi, nayo ni hatua ya uchunguzi juu ya sifa muhtasi zinazohusu uwelewa huu ili tuweze kuthibitisha kuwa zenyewe ni sifa halisi kivitendo na zina uwepo wa nje kihistoria na kisharia, na kuwa kuziamini sifa hizo hakupelekei kutia doa imani wala kutengana na historia. Na sifa hizo ni kama zifuata- zo:

Sifa ya kwanza: Kuzaliwa kwa Imam Mahdi kulitimia katika mazingira ya siri yaliyokuwa ni lazima kutimia.

Ukithibiti uwelewa wa wazo la Mahdi kwa mujibu wa Ahlul-Bait basi inabainika kuwa miongoni mwa sifa barizi mno za lazima za uwelewa huu ni kuzali kwa Imam wa kumi na wawili kuwe kumeambatana na siri na ufi- cho ili baada ya hapo iwezekane kwake ghaibu na kujificha mbali na macho akiwa sehemu yenye amani atakayoichagua Mwenyezi Mungu kwa ajili yake mpaka pale atakapomruhusu kudhihiri.

Hiyo ni kwa kuzingatia kuwa yeye ndiye nyota ya mwisho katika mbingu ya uimamu na Imam ambaye waisilamu hawana Imam mwingine baada yake. Hivyo maana hii inalazimu kupatikana maisha ya uficho, umri mrefu na mazazi ya siri ili nafasi ya uimamu iendelee kutumikiwa muda wote na Imam miongoni ma maimamu kumi na wawili (a.s.) aliye hai aliye ghaibu.

Basi haifai kabisa kusema kuwa: Kwa nini kuzaliwa kwa Imam na kuwe- po kwake baada ya baba yake hayakuwa ni mambo ya wazi yanayoshuhudiwa na kuguswa na kila anayetaka kusadikisha? Kwa sababu laiti ingelikuwa hivyo basi ghaibu na kujificha mbali na macho visingekuwa rahisi kwake kwa sababu yeye ndiye Imam wa kumi na waw- ili, na hatimaye maimamu wangekuwa wengi kuliko idadi hii, na suala hili linapingana na dalili zilizotoka kwa Mtume zilizotajwa mwanzo. Hivyo mazazi ya siri ni miongoni mwa mambo ya lazima yanayotokana na hali halisi ya dalili hizo.

Suala hili linabainisha kuwa kuthibitisha uwepo wa nje wa kadhia ya kuza- liwa Imam Mahdi, kuwepo kwake na maisha yake hakuwezi kukomea tu kwenye uchunguzi wa kihistoria madamu tu tunaamini tangu mwanzo kuwa kadhia hiyo imeambatana na usiri na ufichaji wa kiwango cha juu sana, bali wenyewe ni uthibitisho wa kiakida ndani ya historia ambao ndani yake akida ina nafasi ya msingi, wakati historia yenyewe ina nafasi ya kukamilisha tu.

Kwa sababu sisi tuna yakini tangu mwanzo kuwa wapo wakanushaji wa kadhia hiyo na wenye shaka nayo maadamu tu kadhia ni ya siri iliyofich- wa, na wenye kuitambua ni watu wachache kiasi kwamba inawapa mwanya wengine kuikanusha na kuitilia shaka maadamu tu wako mbali na hali halisi iliyo ya siri iliyofichwa, hali hiyo ni hata kama watakuwa ni ukoo wa karibu na Imam na wafuasi wa dhati, kiasi kwamba lau mtu atawahoji kuhusu kuzaliwa kwa Imam Mahdi, kuwepo kwake na maisha yake wangekanusha, na wao wangewanukulia watu kuwa hawajamwona na wala hawajasikia habari za kuzaliwa na kuwepo kwake.

Hivyo sisi hatuzungumzii suala la kimaada lenye kutambulika vipengele vyake vyote kwa njia ya milango ya fahamu, linalo tutaka tufuate nukuu kamili za historia ili katika uthibitisho wake na ukanushaji wake tuwa- tegemee wanahistoria na wapokezi, hapana si hivyo, bali sisi kimsingi tunazungumzia kadhia ya ghaibu, isipokuwa tu ughaibu huo si ule usio na mipaka, bali wenyewe ni ule wenye miale yenye kutambulika kwa kupitia milango ya fahamu unaofahamika na watu maalumu waliyoteuliwa, hivyo wao wameshuhudia mazazi yake na kuyathibitisha na wameshuhudia ghaibu ndogo na wameithibitisha na wakashuhudia ghaibu kubwa kisha wakaithibitisha. Na kwa ajili hii ndio maana tukasema kuwa uwelewa wa wazo la uwepo wa Mahdi kwa mujibu wa madhehebu ya Ahlul-Bait (a.s.) ni uwelewa wa kiitikadi.

Hii ina maana kuwa kukanusha kwa wakanushaji katika kadhia ya Imam Mahdi hakuwi hoja ya kihistoria ya kimantiki inayoweza kuthibitisha kutokuwepo kwake (a.s.) maadamu tu tumeshaamini tangu mwanzo kuwa kadhia hii ni kadhia ya siri iliyofichwa. Dharura ya uchunguzi wa historia ni kuthibitisha uwepo wa yule aliyemwona Mahdi (a.s.) na akasikia habari za kuwepo kwake na akaziamini, hilo ni bila kujali ukanushaji wa wakanushaji, ukanushaji ambao ni suala la kawaida kupatikana kwenye kadhia ya siri iliyofichwa.

Basi kuanzia hapa tutazama ndani ya uchambuzi wa aina wawili: Kwanza uchambuzi juu ya ushahidi unaothibitisha kuzaliwa kwa Imam na kuende- lea kwake kuwepo. Uchambuzi mwingine ni kuzijadili dalili za wenye kumkanusha (a.s.).

Vielelezo vya kihistoria vinavyothibitisha uwepo wa Imam Mahdi (a.s.)

Upande huu ni mpana mno umejaa namba nyingi sana za vielelezo vya kihistoria, nasi tunavihariri katika nukta mbalimbali:

1. Uthibitisho wa Imam Hasan Al-Askarii (a.s.) kuhusu kuzaliwa mwanae

Imam Mahdi (a.s.):

Katika hilo kuna Hadithi nyingi zilizothibitishwa na Shia na wapokezi wake, nasi tunanukuu baadhi tu:

Hadithi iliyopokewa kutoka kwa Muhammad bin Yahya kutoka kwa Ahmad bin Is’haqa kutoka kwa Abu Hashim Al-Jafariy, amesema: “Nilimwambia Abu Muhammad (a.s.): Heshima yako inanizuia nisiku- ulize, je unaniruhusu nikuulize? Akasema: “Uliza.” nikasema: Ewe bwana wangu! Je, una mtoto wa kiume? Akasema: “Ndiyo.”1

Ndani ya Hadithi hii kuna njia ya upokezi na madhumuni vinavyoji- tosheleza, kwani ni hivi hapa vitabu vya wapokezi vinathibitisha heshima ya Muhammad bin Yahya Abu Jafar At-Tar Al-Qummiy ambaye kaburi lake mpaka leo bado ni maarufu na mashuhuri watu wakilizuru. Pia vinathibitisha hadhi ya juu ya Ahmad bin Is’haqa bin Abdullah bin Saad bin Malik bin Al-Ahwas Al-Ash’ari Abu Ali Al-Qummiy kwa Imam Hasan Al-Askarii (a.s.). Pia vinathibitisha nafasi ya Daud bin Al-Qasim Ibnu Is’haqa bin Abdullah bin Jafar bin Abu Talib Abu Hashim Al-Jafariy…. Kisha tazama uchache wa mtiririko wa wapokezi katika njia ya upokezi wa Hadithi hii, Hadithi ambayo inaonyesha hali ya wahusika kwa ule ufupi wa njia ya upokezi ambao unaheshimika kama ushahidi unaoipa nguvu Hadithi hii.

2. Uthibitisho wa Al-Qabilah

Yeye ni dada wa Imam na shangazi wa Imam na binti wa Imam, anatokana na ukoo wa Ali uliotoharika. Hakimah binti Muhammad Al-Jawwad ni dada wa Imam Al-Had na shangazi wa Imam Al-Askarii, yeye amethibitisha waziwazi kuwa alishuhudia kuzaliwa kwa Imam Mahdi (a.s.) ndani ya usiku aliyozaliwa2, na yeye ndiye aliyesimamia uzazi wa Nargis mama wa Imam Mahdi (a.s.) kwa kupata idhini kutoka kwa baba yake Hasan Al-Askarii (a.s.)3.

3. Uthibitisho wa watu mbalimbali waliomwona Imam (a.s.):

Hapa tuna orodha ndefu ya majina ya watu waliomwona Imam Mahdi na wakakutana naye na wakathibitisha kuwa wamemwona, orodha hiyo ime- sajiliwa na historia na baadhi ya waandishi wameisajili ndani ya vitabu vyao muhtasi, mfano kitabu “Tabsiratul-Waliy Fiman’raa Al-Qaimu Al- Mahdiy” cha Sayyid Hashim Al-Bahrani, humo amewataja watu sabini na tisa waliothibitisha kuwa wamemwona Imam (a.s.) utotoni mwake au kipindi cha ghaibu ndogo, na ametaja majina ya rejea alizozitegemea kati- ka hilo.

Sheikh Abutalibi At-Tajlili At-Tabrizi Zahau yeye amehesabu watu mia tatu na nne waliomwona Imam (a.s.) na wakathibitisha kumwona4.

Sheikh As-Suduq aliyefariki mwaka 381 A.H. na aliyeishi zama za ghaibu ndogo ya Imam Mahdi (a.s.) yeye amehesabu majina ya watu sitini na nne waliothibitisha kuwa wamemwona Imam (a.s.), na wengi miongoni mwao walikuwa mawakala wake5, na wenyewe ni kutoka miji mbalimbali.

Miongoni mwa mawakala wake ni: Kwa watu wa Adhribayjani ni Al- Qasim bin Al-Alau. Kwa watu wa Ahwaz ni Muhammad bin Ibrahim bin Mahziyar. Kwa watu wa Baghdad ni Hajiz Al-Balaliy, Uthman bin Said Al-Amriy, Muhammad bin Uthman bin Said Al-Amriy na Al-Atar. Kwa watu wa Kufa ni Al-Asimiy. Kwa watu wa Qum ni Ahmad bin Is’haqa. Kwa watu wa Nisabur ni Muhammad bin Shadhan. Kwa watu wa Hamdan ni Al-Basamiy, Muhammad bin Abu Abdullah Al-Kufiy Al-Asadiy na Muhammad bin Salih.

Ama wengine waliomwona wasokuwa mawakala wake miongoni mwao ni: Kutoka Isfihan ni Ibnu Bashadhalah. Kutoka Ahwaz ni Al-Huswayniy. Kutoka Baghdad ni Ahmad bin Hasan, Is’haqa mwandishi wa ukoo wa Nawbakhat, Abu Abdullah Al-Khaybariy, Abu Abdullah bin Farukh, Abu Abdullah bin Al-Kindiy, Abul Qasim bin Abu Halis, Abul Qasim bin Dabis, Masrur At-Tabakh mtumwa wa Abu Hasan (a.s.), An-Nayliy na Harun Al-Fazariy.

Kutoka Daynawar ni Ahmad mtoto wa kaka yake na Hasan bin Harun na ami wa Hasan bin Harun. Kutoka Ray ni Abu Jafar Ar-Rafau, Ali bin Muhammad, Al-Qasim bin Musa, mtoto wa Al-Qasim bin Musa, Abu Muhammad bin Harun na Muhammad bin Muhammad Al-Kulayniy.

Kutoka Kazwin ni Ali bin Ahmad na Murdasi. Kutoka Qum ni Hasani bin An-Nadhru, Husayn bin Yaaqub, Ali bin Muhammad bin Is’haq, Muhammad bin Is’haq na Muhammad bin Muhammad. Kutoka Misri ni Abu Rajai. Kutoka Nasibayn ni Abu Muhammad bin Al-Wajnau An- Naswibiy. Kutoka Hamdan ni Jafar bin Hamdan, Muhammad bin Kashmirda na Muhammad bin Harun. Kutoka Yemen ni Ibnu Al-Aajamiy, Al-Jafariy, Hasani bin Al-Fadhlu Ibnu Yazid, baba yake Al-Fadhlu bin Yazid na Shamshati. Pia amewataja waliomwona kutoka Shahruzur, Swaymara, Faris, Qabis na Murwu.

Je, akili inakubali kuwa hawa wote walikubaliana na kuafikiana juu ya kuzua uongo? Ilihali miongoni mwao wapo wasimulizi waaminifu ambao vitabu vya wapokezi wa Hadithi vimethibitisha waziwazi uaminifu wao?

4. Utawala wa koo wa Abbas ulicheza mchezo mchafu juu ya tukio hili

Bila shaka utawala wa ukoo wa Abbas baada ya kufariki Imam Hasan Al- Askarii uliamiliana na familia yake muamala unaoonyesha hofu yao dhidi ya mtoto hatari aliyefichwa dhidi yao, hivyo wakaanza kumtafuta kwa kila nguvu na njia waliyo nayo, kiasi kwamba Al-Muutamid Al-Abbasiy aliye- fariki mwaka 279 A.H alimwamuru mkuu wake wa polisi kuipekua nyum- ba ya Imam Hasan Al-Askarii msako mkali sana huku wakimsaka Imam Mahdi. Akaamuru majirani wa Abu Muhammad wawekwe rumande na familia yake ikamatwe, alifanya hivyo huku akisaidiwa na Jafar mwongo, kwa ajili hiyo watu wa karibu wa Abu Muhammad wakapatwa na kila tati- zo kuanzia kukamatwa, kuwekwa mahabusu, kutishwa, kuvunjiwa heshi- ma na kudhalilishwa.6

Haya yote yalifanywa Imam akiwa na umri wa miaka mitano, wala Al- Muutamid hakujali umri baada tu ya kujua kuwa kijana huyu ndiye Imam Mahdi atakayeangusha jukwaa la muovu kutokana na habari zilizoenea na kutapakaa kuwa Imam wa kumi na wawili wa Ahlul-Bait ataijaza dunia usawa na uadilifu kama itakavyokuwa imejaa dhuluma na ujeuri, hivyo msimamo wake dhidi ya Mahdi ni sawa na msimamo wa Firaun dhidi ya Musa (a.s.) ambaye mama yake alimweka ndani ya mto akiwa mchanga kwa ajili ya kumuogopa Firaun.

Si Al-Muutamid pekee ndiye aliyekuwa amejua ukweli huu bali hata Al- Muutazu na Al-Muhtad waliujua kabla yake, kwa ajili hii Imam Hasan Al- Askari alikuwa katika tahadhari sana ili habari za kuzaliwa Imam Mahdi zisitapakae isipokuwa kati ya watu wateule kutoka kwa mashia wake na wafuasi wake.

Harakati za utawala zimefichua kuwa wenyewe na watu wengine wote walitambua vizuri kuwa Hadithi ya Jabir bin Samra haiwahusu wao wala yeyote aliyetangulia miongoni mwa ukoo wa Umaiya, bali mfano halisi pekee wa Hadithi hiyo ni watu wa nyumba ya utume ambao ni shukio na teremkio la ufunuo.

Kama si hivyo basi ni hatari gani kutoka kwa mtoto asiyevuka umri wa miaka mitano inatishia utawala wao? Kama si kule kuamini kuwa mtoto huyu ndiye yule Mahdi aliyezungumziwa ndani ya Hadithi mbalimbali mutawatiri!

Mmoja wa watafiti anasema: “Ingekuwa kweli hajazaliwa basi kuna maana gani kuwaweka majirani rumande na kutuma vikosi kwenda kuwapekua wanawake wajawazito na kuwapeleleza muda mrefu usiokubalika, kwani mwingine alikuwa chini ya upelelezi muda wa miaka miwili, yalifanywa yote haya huku maswahaba wa Imam Askari wakiteswa na kutumiwa majasusi ili kupeleleza habari za Mahdi (a.s.) na mara kwa mara nyumba zikivamiwa?

Kisha kwa nini utawala haukuridhika na dai la Jafar kuwa kaka yake (a.s.) amefariki bila kuacha mtoto? Hivi haikuwa inatosha kumpa haki yake ya mirathi na mambo yote yaishe kuliko harakati hizi za kipumbavu ambazo zinaonyesha jinsi ulivyokuwa na woga na hofu dhidi ya mwana wa Hasan (a.l.f.s.)?!!

Ndiyo, inaweza kusemwa kuwa nia ya utawala ilikuwa ni kumpa kila mwenye haki haki yake na hiyo ndiyo sababu iliyoupelekea kufuatilia ili kujua uwepo wa mtoto wa kiume ili Jafar asimiliki mirathi peke yake kwa ushahidi wake tu.

Tunasema: Haikufaa kwa utawala wa zama hizo kufatilia jambo hili kwa vitendo hivi vyenye kutia shaka, bali ilipasa Khalifa wa ukoo wa Abbas aliache dai hilo la Jafar mwongo mikononi mwa makadhi, na hasa ukizinga- tia kuwa suala lenyewe ni mirathi, suala ambalo hutokea kila siku mara nyingi, na hapo ingekuwa ni jukumu la kadhi muhusika kufungua mlango wa kuletwa shahidi wa kuthibitisha, kwa mfano angeitwa shangazi yake na Imam Hasan Askari (a.s.) na mama yake na watu wa ukoo wa Hashimu walio karibu na Hasan Askari na kisha asikilize kauli zao achunguze ushahidi wao na hatimaye amaleze kila kitu.

Lakini suala hili kufika kwa mtu wa juu kiutawala na kwa haraka ya namna hii hata kabla Imam Hasan Al-Askari hajazikwa huku suala likitoka kwenye uwezo wa Mahakama ilihali ndiyo yenye jukumu hilo, na kisha utawala unalikabili kwa nguvu kama tuliyoifafanua mwanzo, hayo yote yanathibitisha kwa yakini kuwa utawala ulikuwa ukiamini kwa yakini kabisa kuwa Mahdi tuliyeahidiwa ndiye mzunguko wa mwisho wa cheni toharifu ambayo haiwezi kukatika kwa kufariki Imam wa kumi na moja, hasa baada ya kauli ya (s.a.w.w.) “Hivyo viwili – Kitabu na Kizazi – hav- itoachana mpaka vitakaponifikia kwenye Hodhi.” kuenea kwa watu wote.

Kwani kutokuzaliwa Mahdi au kutoendelea kuwa hai maana yake ni kutoweka kwa kizazi, na hii ni kauli isiyosemwa na yeyote yule anayejiita kiongozi wa waumini miongoni mwa wana wa Abbas, kwa sababu kauli hiyo ni kumkadhibisha Mtukufu Mtume wetu (s.a.w.w.) bali haisemwi na mwisilamu yeyote ila yule tu asiyejali ukadhibishaji huu au mwenye kuji- danganya kuwa anaawili Hadithi na kuyapeleka malengo ya Hadithi kwenye kitu ambacho hakijaletewa hoja yoyote ya wazi.”7

5. Wanachuoni wa Sunni wamekiri kuwa Imam Mahdi (a.s.) ameshaz- aliwa.

Sayyid Thamir Al-Amidiy amezungumzia suala hili akasema: “Kauli za kukiri za Wanachuoni wa sharia, wafasiri, wanahistoria, watafiti, wafasihi na waandishi wa kisunni zimefikia zaidi ya mia moja, wote wakikiri wazi- wazi kuwa Imam Mahdi (a.s.) ameshazaliwa. Zaidi ya nusu yao wametam- ka waziwazi kuwa Imam Muhammad bin Hasan Al-Mahdi (a.l.f.s.) ndiye Imam tuliyeahidiwa kuwa atadhihiri mwishoni mwa zama.

Kauli hizi za kukiri zimepangwa kulingana na vifo vya wenye nazo, hivyo tumezikuta zimeungana kizama kiasi kwamba haishindikani mwenye tamko la sasa kuwepo zama za mwenye tamko lililopita, hivyo ni kuanzia zama za ghaibu ndogo mpaka leo hii, ishaallah tutataja kauli za baadhi yao ambazo tumezipata ndani ya vitabu vyao pindi zamu yao itakapofika, na kwa wengine tutaishia kutaja majina yao tu bila kugusia kauli zao hiyo ni kutokana na kushindikana kuzinukuu katika sura hii.

Kauli zao zimefikia ishirini na tisa huku ya mmoja kati yao ikiwemo ndani ya kitabu “Ilzamun-Naswibu” kwenye kurasa zaidi ya mia moja.8 Je hali ingekuwaje laiti angesajili kauli zao wote? Zaidi ya hapo ni kuwa tutakayo itaja kwenye matamshi bila kuonyesha rejea yake kwenye pambizo ni dalili kuwa tumeichukua kutoka kwenye vitabu vya Shia Imamiya ambavyo vimetangulia kuzungumzia suala hili, na tutakazania kusajili namba ya juzuu, namba ya kurasa, sehemu na mwaka wa chapa.

Kitabu kikubwa mno katika mlango huu ni kitabu “Al-Mahdiyyu Al- Muntadhar Finahjil-Balagha” cha Sheikh Mahdiyyu Faqihi Iymaniy, ambaye humo ametaja wapokezi mia wawili na wawili miongoni mwa wapokezi wa kisuni ambao wamekiri hilo9 huku akiishia kutaja majina yao na vitabu vyao kwa kuainisha juzuu zake pamoja na kurasa zake bila kugusia kauli zao.

Nyakati nyingine alilazimika kuainisha kwa umakini kiunganishi kati yake na wao, na yaliweza kumpita karibuni majina thelathini. Sana tumemtege- mea yeye na wala hatukurudia tena ili kutafuta chochote kilichompita kwani tayari kuna mwingine asiyekuwa mimi alisharudia na kukusanya kile kilichompita10, akarudia kwa mzunguko katika dalili hii huku akiishia kukusanya na kupangilia kulingana na karne.”11

Kisha akataja majina mia moja ishirini na nane ya waandishi miongoni mwa waandishi wa kisunni ambao ndani ya baadhi ya vitabu vyao wamem- taja Imam Mahdi kwa kichwa cha habari: Imam wa kumi na wawili mion- goni mwa maimamu wa Ahlul-Bait (a.s.). Miongoni mwa waandishi hao wamo walioishi zama za kuzaliwa kwake na zama za ghaibu ndogo, ushahidi wa hawa una hadhi maarufu ya kihistoria.

Miongoni mwa hao ni:

1. Abubakri Ar-Riwayaniy, Muhammad bin Harun aliyefariki mwaka 307
 A.H ndani ya kitabu chake “Al-Musnad”.

2. Ahmad bin Ibrahim bin Ali Al-Kindiy, yeye ni kati ya wanafunzi wa
 Ibnu Jarir At-Tabari aliyefariki mwaka 310 A.H.

3. Muhammad bin Ahmad bin Abu Thalji, Abubakri Al-Baghdadiy aliye- fariki mwaka 322 A.H. ndani ya kitabu “Mawalidul-Aimah”, hiki kimechapwa ndani ya kitabu “Al-Fusulul-Asharat Fil-Ghaybah” cha Sheikh Al-Mufid, pamoja na kitabu “Nawadiru Ar-Rawandiy kili- chochapwa Najaf tukufu mwaka 1370 A.H. Na miongoni mwa Wanachuoni wakubwa waliokuwa karibu na zama za kuzaliwa kwake ni Al-Khuwarazimiy aliyefariki mwaka 387 A.H. ndani ya kitabu chake “Mafatihul-Ulumi: 32 na 33” chapa ya Lidan mwaka 1895 A.D.


16:38 - 11/05/2017    /    Number : 677729    /    Show Count : 250


Users Comment
No Comment for this news
Your Comment
Name :
E-mail : 
*Comments :
Captcha:
 

Search
Advance Search Web Search
banners
Kiongozi Muadhama

Imam

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

presstv

Radio Tehran

Al-hikma

Iqna

Irna

Mubaligh

Jamiatul Mustafa (SAWW

Islamica

Rayhanee
vote
Disable
UsersStats
Visitorsofpage: 27702
Visitorsofday : 49
Visitorsofpage : 70535
Onlinevisitors : 1
PageLoad : 1.4531

Home|Habari|Kutuhusu|Programu|Historia ya mahusiano ya kitamaduni|Mahusiano ya jumuia zingine |Machapisho|Ushirikiano na Maktaba zingine|Matukio ya Kiutamaduni|Ofisi zingine za Iran