Saturday, March 23, 2019 Home|Habari|فارسي|Kiswahili
 

Nyumbani|Uislamu|Lugha ya Kifursi|FAQ|Wasiliana nasi|Links|Sitemap
Title
iran
.
Login
Username :   
Password :   
 
Captcha:
[Signup]
NewsletterSignup
Name :   
E-mail :   


  Print        Send to Friend

Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete azindua rasmi tamasha la ZIFF 2017, Atunukiwa tuzo ya mtu aliyetukuka

Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete azindua rasmi tamasha la ZIFF 2017, Atunukiwa tuzo ya mtu aliyetukuka Rais Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Jumamosi usiku wa Julai 8,2017, amezindua rasmi tamasha la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF), tukio lililofanyika Ngome Kongwe, Mjini Unguja-Zanzibar. Katika tukio hilo, Dkt. Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo la 20, tokea kuanzishwa kwake miaka 20, iliyopita.

 Ambapo uongozi wa ZIFF waliweza kusoma wasifu wa Rais huyo Mstaafu kwa namna alivyoweza kusaidia mchango mkubwa kuendeleza tasnia ya filamu nchini na sanaa kwa ujumla huku akiwa ndio kiongozii wa juu kabisa hapa nchini kuizungumzia mara kwa mara tamasha hilo la ZIFF. Akizungumza wakati wa ufunguzi rasmo, Dkt. Jakaya Kikwete alishukuru na kupongeza kwa mafanikio waliyopata ZIFF hadi kufikia msimu wa 20, tokea kuanzishwa kwake ambapo imewataka waendelee zaidi na zaidi. “Nashukuru kwa kunialika.

Nashukuru kwa tuzo hii kwani sikutegemea na nina wapongeza kwa mafanikio haya ua kutimiza miaka 20. Nawaombeeni muendelee miaka 20 na 20 zaidi vizazi na vizazi mpaka litakapofika mwisho” alieleza Dkt. Kikwete. Dkt. Kikwete alitoa ushahuri kwa uongozi wa ZIFF kuwa na kifua mbele kwa namna filamu zinazopita kwenye tamasha lao kuzifuatilia kwani zimekuwa zikifanya vizuri huko mbele ikiwemo tuzo za Hollywood. Kwani ZIFF imekuwa ni taasisi yenye nafasi muhimu kwa jamii ya watu wa Zanzibar Tanzania .

Kwa sasa ni kujipima katika miongo miwili hii ni jinsi gani na kiasi gani ZIFF ilivyojisogeza na kuwa karibu na jamii” alieleza Dkt. Kikwete. Aidha, Dkt. Kikwete alieleza kuwa, tasnia ya sanaa hapa nchini inatakiwa ipande na kuwa juu ili kuendeleza utamaduni wa Mzanzibar na Mtanzania inaenda vipi. Pia amewataka ZIFF kuwa karibu na jamii ili kuweza kujenga ushawishi kwa jamii hiyo na kilamwaka wawe na matamanio zaidi ya tamasha.

Awali akitangaza tuzo hiyo, Mwenyekiti wa ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo mbele ya jopo la wajumbe wa Bodi ya ZIFF, waliweza kumtangaza rasmi Dkt. Kikwete kutwaa tuzo hiyo kubwa kabisa ambayo utolewa kwa watu wenye kutukuka ambao pia wameifanya mchango mkubwa ndani na nje katika masuala ya Sanaa na tasnia ya filamu. Mwenyekiti wa ZIFF Mahmoud Thabit Kombo aliweza kuwataka wazawa hasa Wazanzibar kuwa na mwamko wa kuthamini cha kwao na hata kujitokeza kudhamini tamasha hilo. “ZIFF imefungua milango yake wazi kwa mtu yeyote kujitokeza na kudhamini tamasha hili. Wazawa tunawakaribisha sana kwani uwepo wa tamasha ili ndio kukuwa kwa uchumi wetu na maendeleo hivyo tujisikie fahari kwa uwepo wake”. Ameeleza Mahmoud Thabit Kombo. Akiwa mgeni rasmi, Dkt. Kikwete aliweza kushuhudia filamu ya uzinduzi wa tamasha hilo ya ‘T-Junction’ iliyoandaliwa na mtayarishaji wake Amir Shivj kutoka Kijiweni Production ya Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo, Ngome Kongwe iliweza kufurika umati mkubwa waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo.

Imeelezwa kuwa, wageni kutoka mataifa mbalimbali zaidi ya 14,000 wamefika Visiwani Zanzibar huku hoteli mbalimbali zikiwa zimepata faida kwa kipindi hiki, alieleza Mwenyekiti wa ZIFF, Mh. Mahmoud Thabit Kombo ambapo ameweka wazi kuwa katika orodha yao ya wageni kutoka Mataifa mbalimbali huku wengine wakiendelea kufika kila siku. Tamasha hilo linatarajia kumalizika hadi Julai 16,2017. Huku kila siku kukiwa na filamu zinazoonyeshwa Ngome Kongwe na zingine zikioneshwa kwenye kumbi mbalimbali ndani ya viunga vya Unguja pamoja na Vijiji vya Zanzibar sambamba na kutoa mafunzo ya uendeshaji wa filamu na mafunzo mbalimbali katika tasnia hiyo ya filamu


12:49 - 12/07/2017    /    Number : 682218    /    Show Count : 216


Users Comment
No Comment for this news
Your Comment
Name :
E-mail : 
*Comments :
Captcha:
 

Search
Advance Search Web Search
banners
Kiongozi Muadhama

Imam

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

presstv

Radio Tehran

Al-hikma

Iqna

Irna

Mubaligh

Jamiatul Mustafa (SAWW

Islamica

Rayhanee
vote
Disable
UsersStats
Visitorsofpage: 27693
Visitorsofday : 37
Visitorsofpage : 70523
Onlinevisitors : 2
PageLoad : 1.6094

Home|Habari|Kutuhusu|Programu|Historia ya mahusiano ya kitamaduni|Mahusiano ya jumuia zingine |Machapisho|Ushirikiano na Maktaba zingine|Matukio ya Kiutamaduni|Ofisi zingine za Iran