Saturday, March 23, 2019 Home|Habari|فارسي|Kiswahili
 

Nyumbani|Uislamu|Lugha ya Kifursi|FAQ|Wasiliana nasi|Links|Sitemap
Title
iran
.
Login
Username :   
Password :   
 
Captcha:
[Signup]
NewsletterSignup
Name :   
E-mail :   


  Print        Send to Friend

Ustawi wa sayansi na teknolojia Iran ni kwa malengo ya amani

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, ustawi wa sayansi na teknolojia nchini Iran unafanyika kwa malengo ya amani na kibinadamu na katu hakuna malengo yasiyo na kimaadili na haribifu.

Ishaq Jahangiri Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran aliyasema hayo Jumamosi mjini Tehran katika kikao cha kufunga Kongamano la Tatu la Kimataifa la Seli Shina. Aliongeza kuwa, katika kadhia ya nyuklia, Iran imetuhumiwa pasina haki na sasa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki, IAEA, umetoa ripoti kadhaa ambazo zimethibitisha kuwa shughuli za nyuklia za Iran zinafanyika kwa malengo ya amani.

Jahangiri ameashiria vikwazo vya kidhalimu vya Marekani dhidi ya Iran na kusema: "Wairani wamebadilisha vitisho kuwa fursa na hawataruhusu vizingiti vyovyote katika mkondo wao wa ustawi wa sayansi na teknolojia."

 

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa, Iran ina nguvu kazi yenye masomo ya juu na ya kipekee. Ameongeza kuwa, Iran inakaribisha ushirikiano na vituo muhimu vya sayansi na teknolojia duniani.

Pembizoni mwa mkutano huo kulizinduliwa mafanikio ya hivi karibuni ya Iran katika uga wa seli shina na tiba.

Kongamano la Tatu la Kimataifa la Seli Shina lilianza Jumatano mjini Tehran na limemaliza shughuli zake Jumamosi.

 


12:31 - 13/12/2018    /    Number : 719790    /    Show Count : 50


Users Comment
No Comment for this news
Your Comment
Name :
E-mail : 
*Comments :
Captcha:
 

Search
Advance Search Web Search
banners
Kiongozi Muadhama

Imam

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

presstv

Radio Tehran

Al-hikma

Iqna

Irna

Mubaligh

Jamiatul Mustafa (SAWW

Islamica

Rayhanee
vote
Disable
UsersStats
Visitorsofpage: 27689
Visitorsofday : 31
Visitorsofpage : 70517
Onlinevisitors : 1
PageLoad : 0.9531

Home|Habari|Kutuhusu|Programu|Historia ya mahusiano ya kitamaduni|Mahusiano ya jumuia zingine |Machapisho|Ushirikiano na Maktaba zingine|Matukio ya Kiutamaduni|Ofisi zingine za Iran