Saturday, March 23, 2019 Home|Habari|فارسي|Kiswahili
 

Nyumbani|Uislamu|Lugha ya Kifursi|FAQ|Wasiliana nasi|Links|Sitemap
Title
iran
.
Login
Username :   
Password :   
 
Captcha:
[Signup]
NewsletterSignup
Name :   
E-mail :   


  Print        Send to Friend

Rais Rouhani: Vikwazo vya kidhalimu vya Marekani dhidi ya Iran, ni hatua ya kigaidi kwa asilimia mia moja

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameyasema hayo leo katika mkutano wa pamoja na waandishi wa habari aliofanya na mwenyeji wake Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki mjini Ankara. 

Rais Rouhani amefafanua kuwa: Azimio nambari 2231 linazitaka nchi zote duniani ziunge mkono makubaliano ya nyuklia ya Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) na kuandaa mazingira mwafaka kwa ajili ya kustawisha uhusiano wa kibiashara na Iran.

Rais wa Iran amesema: Leo kuna nchi chache duniani ambazo zimeungana na Marekani kupuuza haki za wananchi wa Iran kwa kukiuka azimio hilo la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pamoja na sheria za kimataifa. Ameongeza kuwa, enzi za ubabe na ujabari duniani zimefikia tamati, na mataifa yanataka yajichukulie maamuzi yenyewe kwa kuzingatia manufaa na maslahi yao ya pamoja.

Rais Hassan Rouhani wa Iran (kushoto) akiamkiana na Rais Recep Tayyip Erdoğan wa Uturuki walipokutana kwa mazungumzo ya pande mbili mjini Ankara

Rais Rouhani aidha amemshukuru Rais Erdogan na serikali ya Uturuki kwa misimamo thabiti na ya wazi waliotangaza kuhusiana na vikwazo vya kidhalimu vya Marekani dhidi ya Iran na kuongeza kuwa: Misimamo hii ya kukabiliana na hatua za upande mmoja na vikwazo haramu dhidi ya Iran inaonyesha jinsi nchi mbili za Iran na Uturuki zinavyofungamana na sheria na maadili.

Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amezungumzia pia mgogoro wa Syria na kueleza kwamba, nchi mbili za Iran na Uturuki zinaitakidi kuwa, matatizo ya Syria inapasa yatatuliwe na wananchi wa nchi hiyo sambamba na kulindwa umoja wa ardhi yake yote.

Kuhusiana na masuala ya Yemen, Rais wa Iran amesema, mtazamo wa Tehran na Ankara ni kutatuliwa mgogoro wa nchi hiyo kupitia mazungumzo baina ya Wayemeni wenyewe na akaongeza kuwa, Iran na Uturuki zitaendelea kufanya juhudi za kutuma misaada ya kibinadamu kwa wananchi wa nchi hiyo.../

 


12:11 - 21/12/2018    /    Number : 720281    /    Show Count : 46


Users Comment
No Comment for this news
Your Comment
Name :
E-mail : 
*Comments :
Captcha:
 

Search
Advance Search Web Search
banners
Kiongozi Muadhama

Imam

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

presstv

Radio Tehran

Al-hikma

Iqna

Irna

Mubaligh

Jamiatul Mustafa (SAWW

Islamica

Rayhanee
vote
Disable
UsersStats
Visitorsofpage: 27700
Visitorsofday : 45
Visitorsofpage : 70531
Onlinevisitors : 1
PageLoad : 1.3594

Home|Habari|Kutuhusu|Programu|Historia ya mahusiano ya kitamaduni|Mahusiano ya jumuia zingine |Machapisho|Ushirikiano na Maktaba zingine|Matukio ya Kiutamaduni|Ofisi zingine za Iran