Thursday, December 13, 2018 Home|Habari|فارسي|Kiswahili
 

Nyumbani|Uislamu|Lugha ya Kifursi|FAQ|Wasiliana nasi|Links|Sitemap
Title
iran
.
Login
Username :   
Password :   
 
Captcha:
[Signup]
NewsletterSignup
Name :   
E-mail :   


Salam za Mapinduzi ya Kiislamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema februar 11 ni siku muhimu ya maadhimisho ya mapinduzi ya Kiislamu ya Iran hivyo anahamasisha Waislamu kuadhimisha siku hiyo Dk. Bagheri alisema hayo Dar es salam jana alipokuwa anazungumza na waandihsi wa habari kuhusiana na maadhimisho hayo. Ni muhimu kuwakumbusha kuwa Mapinduzi ya Kiislamu yanaendeleza shughuli zake katika mazingira ambayo nguvu za pamoja zinajaribu kushindana na Mapinduzi hayo na kutumia mbinu mbalimbali. februari 11 kila mwaka ni kumbukumbu za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ambazo zinafanyika kila mwaka , ambao ushindi huo ulipatikana mwaka 1979 chini ya uongozi wa Imam Khomeni (ra) mwasisi mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yalifanikiwa kuupindua utawala hasimu na wakidikteta wa Pahlavi Shah alisema,
 10:59 - 8/02/2018 - Comments : 0More >>
Kongamano la Amani Dar
Kongamano la wafuasi wa dini mbalimbali kuishi kwa masikilizano na kuhus mahusiano na mashirikiano ya dini mbali katika kukabilia na wahafidhina kwa watu wa dini limefanyika katika Kituo cha Utamadni cha Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Dar es Salaam nchini Tanzania. Kongamano hilo ambalo lilifanyika tarehe 14- 11- 2017 limeandaliwa kwa ushirikiano wa Kituo cha Kiutamaduni cha Iran nchini Tanzania na Baraza la Dini kwa ajili ya Amani . Akihutubia katika kongamano hilo, Rose Muzala, Mkuu wa Kitivo cha Sayansi za Jamii cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amesema, dini bila ya akili na mantiki ina madhara, na akili tupu bila ya dini haina ufanisi. Aidha ametoa shukurani kwa kituo cha Kiutamaduni cha Iran nchini Tanzania. Mussa Farhang, balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania ambaye alikuwa mzungumzaji mwengine katika kongamano hilo, amesema kuishi kwa masikilizano wafuasi wa dini mbalimbali katika Jamhuri ya Kiislamu kuna chimbuko la kihistoria; na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umejumuisha pamoja dini na akili. Mbali na kupongeza hali ya kuishi kwa masikilizano iliyopo baina wa waumini wa dini mbalimbali nchini Tanzania, Farhang ameongeza kuwa hitilafu za kidini ni jambo la kawaida, lakini inachopasa kufanya ni kutilia mkazo nukta za pamoja badala ya hitilafu. Mjumuiko wa viongozi wa Waislamu na Wakristo Tanzania Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania amesisitiza kuwa wanaofanya jinai kwa jina la dini ni watu wasio na akili timamu; na njia pekee ya kuwezesha wafuasi wa dini tofauti kuishi kwa masikilizano ni kujiepusha na vitendo vya machafuko na ukatili. Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Zanzibar, Rashid Ali Juma, yeye ameashiria historia ya pamoja ya Iran na Tanzania na kusisitiza azma ya Zanzibar ya kuimarisha uhusiano baina ya pande mbili. Kongamano hilo limehudhuriwa pia na wahadhiri pamoja na wanachuo wa nchini Tanzania…/
 12:40 - 22/11/2017 - Comments : 0More >>
Ujumbe wa Hijja Mwaka 2017
Ninamshukuru Mwenyezi Mungu Mkubwa ambaye mwaka huu pia amewapa waumini kutoka maeneo mbalimbali ya dunia, saada na ufanisi wa kutekeleza ibada ya Hija ili wafaidike na chemchemi hiyo yenye maji matamu na yanayotiririka, na kufanya itikafu na kuwa kandokando ya Nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu katika nyakati za ibada, khushui, dhikri na kujikurubisha kwake katika siku na nyusiku zinazohesabika kuwa ni fursa adhimu na yenye baraka ambazo saa zake ni mithili ya mada inayofanya muujiza unaoweza kubadilisha nyoyo na kutakasa na kuzipamba nafsi na roho zao. Hija ni ibada yenye siri nyingi, na nyumba tukufu (ya al Kaaba)
 11:23 - 05/09/2017 - Comments : 0More >>
Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete azindua rasmi tamasha la ZIFF 2017, Atunukiwa tuzo ya mtu aliyetukuka
Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete azindua rasmi tamasha la ZIFF 2017, Atunukiwa tuzo ya mtu aliyetukuka Rais Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Jumamosi usiku wa Julai 8,2017, amezindua rasmi tamasha la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF), tukio lililofanyika Ngome Kongwe, Mjini Unguja-Zanzibar. Katika tukio hilo, Dkt. Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo la 20, tokea kuanzishwa kwake miaka 20, iliyopita. Ambapo uongozi wa ZIFF waliweza kusoma wasifu wa Rais huyo Mstaafu kwa namna alivyoweza kusaidia mchango mkubwa kuendeleza tasnia ya filamu
 12:49 - 12/07/2017 - Comments : 0More >>
Habari 24 blog
SHEIKH JALALA AONGEA NA (UN) KUHUSU AMANI YA PALESTINA
Kiongozi wa Dhehebu la SHIA Ithna Sheria Sheikh Hemed Jalala ameitaka jumuiya umoja wa mataifa (UN) kuiangalia kwa jicho la karibu nchi ya Palestina ili amani iwezekurejea kama ilivyo kwa nchi ya Tanzania. Sheikh Hemed Jalala ameyasema hayo leo katika semina ya Quds ya kuwakumbuka waislamu na wote wanaoishi kwa kupata taabu nchini Palestina, ambapo ameeleza kuwa watanzania inabidi waoneshwe kusikitishwa na kupinga vikali dhidi ya mambo yanayoendelea nchini humo kwani kinamama wanakosa huduma za afya jambo linalopelekea kujifungua kwa taabu. Sheikh Jalala amefafanua kuwa hali ya nchi hiyo siyo nzuri kwani vijana wa kiislamu wamekuwa wakizuiwa kuswali kwenye
 11:10 - 19/06/2017 - Comments : 0More >>
Semina"Mchango wa Imam Khomein (r.a) Ulimwenguni yafanyika Dar es salaam
Balozi wa Iran Nchini Tanzania Mhe.Mussa Farahang akitoa mada katika Semina ya Mchango wa Imam Khomein (r.a) Ulimwenguni, Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es alaam.
 10:20 - 6/06/2017 - Comments : 0More >>
uchaguzi wa Iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza juu ya udharura wa wananchi wa Iran kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa leo. Rouhani asema mahudhurio makubwa yataimarisha izza, usalama wa Iran May 19, 2017 07:45 Rais Hassan Rouhani wa Iran ametoa wito kwa wananchi kushiriki kwa wingi katika uchaguzi wa rais unaofanyika hii leo hapa nchini akisisitiza kuwa, mahudhurio makubwa katika zoezi hilo yataimarisha izza na usalama wa Jamhuri ya Kiislamu. Wananchi wa Iran leo wanashiriki katika uchaguzi wa Urais May 19, 2017 04:22 Wananchi wa Iran waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wanaelekea katika masanduku ya kupigia kura kwa ajili ya kumchagua Rais wa nchi. Uchaguzi wa Rais wa Iran kufanyika katika nchi 102 duniani May 18, 2017 15:26 Mkuu wa kamati ya kusimamia uchaguzi wa 12 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nje ya nchi amesema kuwa, uchaguzi huo utafanyika katika nchi 102
 12:57 - 19/05/2017 - Comments : 0More >>

<< Previous1 2 3 4 5 6 7 8 Next Page >>

Search
Advance Search Web Search
banners
Kiongozi Muadhama

Imam

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

presstv

Radio Tehran

Al-hikma

Iqna

Irna

Mubaligh

Jamiatul Mustafa (SAWW

Islamica

Rayhanee
vote
Disable
UsersStats
Visitorsofpage: 13288
Visitorsofday : 2
Visitorsofpage : 63955
Onlinevisitors : 1
PageLoad : 1.0781

Home|Habari|Kutuhusu|Programu|Historia ya mahusiano ya kitamaduni|Mahusiano ya jumuia zingine |Machapisho|Ushirikiano na Maktaba zingine|Matukio ya Kiutamaduni|Ofisi zingine za Iran