Thursday, December 13, 2018 Home|Habari|فارسي|Kiswahili
 

Nyumbani|Uislamu|Lugha ya Kifursi|FAQ|Wasiliana nasi|Links|Sitemap
Title
iran
.
Login
Username :   
Password :   
 
Captcha:
[Signup]
NewsletterSignup
Name :   
E-mail :   


BI FATMA (AS): Kielelezo cha nguvu ya mwanamke muasisi wa uchumi
WAISLAMU wameadhimisha siku ya kuzaliwa kwa Fatma, mtoto wa Mtume Mohammad A.S kwa kuwahamasisha wanawake kufuata yale aliyokuwa akiyafanya yakiwemo ya kiuchumi. Anapozungumziwa Bi Fatma A.S anamzungumziwa mwanamke ambae ni kioo cha kiwiliwili ambacho si wanawake tu wanaweza kujitazama na kurekebisha tabia na maadili yao, bali hata mamia ya wanaume wengi mbali ya mitume na manabii wa Mungu. Huyu ni mtoto wa Mtume Muhammad S.A.W ambae alitumwa kufundisha maadili, tabia njema, upendo na mahusiano mema baina ya binadamu wa rangi na dini zote. Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Dk. Ali Bagheri akimzungumzia Fatma wakati maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa mwishoni mwa wiki anasema mwanamke huyo alilelewa katika nyumba bora miongoni mwa nyumba bora kabisa kuwahi kutokea katika mgongo wa dunia, nyumba ambayo ilichomoza duru iliyomfunza binadamu utu na ubidamu kamili, nuru ambayo ilimkataza Muarabu wa zama zile kuua mtoto wa kike kama ilivyokua ada yao, nuru iliyomuekea mipaka binadamu huyo
 13:37 - 5/04/2016 - Comments : 0More >>
“Islamic Revolution of Iran eliminated all imported ‘isms’
On 11th February this year, the Islamic Republic of Iran celebrated its 37th Anniversary of the Revolution. It was the time when the people of Iran dethroned the biggest despotic ruler of the region (Persian Gulf), Mohammad Reza Pahlavi Shah and established the Islamic republic system in the country. Our Staff Writer JAFFAR MJASIRI was granted an exclusive interview by the Cultural Counsellor, Mr Ali Bagheri, recently, who among other things, said that Iran’s Revolution rivalled out all the imported `isms’.
 11:01 - 18/02/2016 - Comments : 0More >>
Mapinduzi ya Kiislamu; kigezo cha kuiga katika kukabiliana na siasa za kibeberu za Magharibi
Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran ni moja ya matukio makubwa zaidi ya karne ya 20; na likiwa moja ya matukio yasiyo na mfano wake katika zama hizi yalifungua ukurasa mpya katika historia ya mwanadamu na kuwa chemchemi ya mabadiliko makubwa katika nyuga za kiutamaduni, kisiasa, kijamii na kiuchumi. Mapinduzi ya Kiislamu kwa wananchi wa Iran lilikuwa ni hitajio na jambo la lazima, ambalo liligeuka kuwa mwanzo wa harakati mpya katika uga wa muqawama wa mataifa, katika kukabiliana na mifumo na tawala za kibeberu. Na ndiyo maana ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ulikuwa ni tukio ambalo mwangwi wake ulivuka mpaka wa kieneo. Kimsingi, kila Mapinduzi yanayojiri katika eneo la kijiografia la watu huwa na athari na kusababisha mageuzi na mabadiliko ya msingi; lakini kitu kinachoyalinda mapinduzi hayo na kuyafanya yadumu ni upana na ukubwa wa taathira zake. Sifa hii imeonekana kwa uwazi kabisa na kwa kiwango kikubwa katika Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran; kiasi kwamba mataifa mengi ya wanyonge duniani yalihisi kuwa yataweza kupata matamanio na matarajio yao kwa kufuata kigezo cha Mapinduzi ya Kiislamu. Ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ulivuruga mlingano uliokuwa
 10:58 - 8/02/2016 - Comments : 0More >>
Bwana Baqeri Kukutana na wa waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania ametaka kuimarishwa uhusiano wa nchi hiyo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika sekta ya utalii. Nape Nnauye ameeleza kuridhishwa na kutiwa saini makubaliano ya kiutamaduni kati ya nchi mbili hizo na kubainisha kuwa kustawisha uhusiano wa sekta ya utalii kati ya Iran na Tanzania ni muhimu sana kwa nchi mbili hizo na amelipokea vizuri suala la kupewa mafunzo wasanii wa Tanzania nchini Iran. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wa Tanzania ameyasema hayo katika mazungumzo na Ali Bagheri mshauri wa Masuala ya Utamaduni kutoka Kituo cha Utamaduni cha Iran jijini Dar es Salaam Tanzania.
 11:40 - 18/01/2016 - Comments : 0More >>
Madhehebu ya kiislam Nchini kote na duniani wametakiwa kujenga umoja wa kudumu,
Madhehebu ya kiislam Nchini kote na duniani wametakiwa kujenga umoja wa kudumu,kukaa kwa pamoja na kujadili maswala yanayowahusu jambo ambalo litasaidia kuleta amani baina ya dini ya Kiislam na dunia kwa ujumla. Rai hiyo imetolewa Jijini Dar es salaam na sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Sheikh Alhadi Mussa Salim wakati wa sherehe ya maalum ya mauled iliyowakutanisha waislam wa Madhehebu ya SHIA na SUNNI kwa ajili ya kusherekea na kukumbaka kwa pamoja siku ya kuzaliwa kwa mtume muhammad (s.a.w.w), Masjid Udoe Jijini Dar es salaam.
 11:34 - 18/01/2016 - Comments : 0More >>
Waislamu walaani kuuawa Sheikh Nimr
Waislamu kote duniani wanaendelea kulaani kutekelezwa hukumu ya kuuawa mwanazuoni maarufu wa Kiislamu Saudi Arabia Sheikh Nimr Baqir Al Nimr. Nchini Kenya Jumuiya ya Waislamu ya Mahdi imetoa taarifa na kulaani hatua ya utawala wa ukoo wa Aal Saud kutekeleza hukumu ya kumuua kiongozi huyo wa Kiislamu. Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Abdulqadir Nasser amesema, "Kosa pekee alilofanya Shahid Sheikh Nimr ni kuukosoa vikali utawala dhalimu na haramu wa Saudia na silaha yake pekee ilikuwa ni mantiki na kusema ukweli." Amesema utawala wa Saudia umekataa kusikiliza mantiki ya Shahid Sheikh Nimr; na sawa na tawala zingine za kiimla na kidhalimu, jibu la mantiki limekuwa ni kuzima sauti hiyo. Abdulqadir Nasser amesema kuuawa Sheikh Nimr ni ishara ya misingi ya kidhalimu na umwagaji damu ya utawala wa Saudia ambao kwa itikadi yake ya Kiwahabi umeibua makundi ya kigaidi kama vile ISIS, Al Qaeda, Boko Haram na Al Shabab.
 10:13 - 4/01/2016 - Comments : 0More >>
Maulidi Saidi
Msingi wa Umoja wa Kiislamu katika Qurani na Sira ya Mtume SAW
Tuko katika siku tukufu za kuadhimisha Maulid ya Mtume Mtukufu wa Uislamu Mohammad al Mustafa SAW. Waislamu wa madhehebu ya Sunni wanaadhimisha siku hiyo tarehe 12 Rabiul Awwal na Waislamu wa Madhehebu ya Shia wanamini siku hiyo ni tarehe 17 Rabiul Awwal. Miaka mingi iliyopita, Hayati Imam Khomeini MA, Kiongozi mwanzilishi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ambaye binafsi alikuwa mstari wa mbele kulingania umoja wa Kiislamu alipendekeza kuwa, muda uliopo baina ya tarehe hizo mbili uwe ni "Wiki ya Umoja wa Waislamu" kwa lengo la kuimarisha mashikamano na udugu baina ya madhehebu za Kiislamu. Kwa hivyo wiki hii ni fursa munasibu ya kukutana na kuchunguza udharura wa daima wa kuwepo umoja wa Kiislamu hasa katika kipindi hiki cha fitina na ghasia. Waislamu wa madhehebu mbali mbali wanahitilafiana
 10:23 - 23/12/2015 - Comments : 0More >>

<< Previous1 2 3 4 5 6 7 8 Next Page >>

Search
Advance Search Web Search
banners
Kiongozi Muadhama

Imam

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

presstv

Radio Tehran

Al-hikma

Iqna

Irna

Mubaligh

Jamiatul Mustafa (SAWW

Islamica

Rayhanee
vote
Disable
UsersStats
Visitorsofpage: 13289
Visitorsofday : 3
Visitorsofpage : 63956
Onlinevisitors : 1
PageLoad : 1.1250

Home|Habari|Kutuhusu|Programu|Historia ya mahusiano ya kitamaduni|Mahusiano ya jumuia zingine |Machapisho|Ushirikiano na Maktaba zingine|Matukio ya Kiutamaduni|Ofisi zingine za Iran