Monday, November 19, 2018 Home|Habari|فارسي|Kiswahili
 

Nyumbani|Uislamu|Lugha ya Kifursi|FAQ|Wasiliana nasi|Links|Sitemap
Title
iran
.
Login
Username :   
Password :   
 
Captcha:
[Signup]
NewsletterSignup
Name :   
E-mail :   

matukio ya siku tasua na ashuraa mwaka 2018


matukio ya siku tasua na ashuraa mwaka 2018

 12:20 - 21/09/2018More >>

Masiku ya mwanzo ya mwezi Muharram
Assalam Alaykum Warahmatullah Wabarakatuh. Hamjambo wapenzi wasikilizaji na karibuni kuwa nasi katika kipindi hiki maalumu kinachokujieni kwa mnasaba wa kuanza mwezi mtukufu wa Muharram na harakati ya Bwana wa Vijana wa Peponi Imam Hussein bin Ali (as). Ni matarajio yangu kuwa mtaendelea kuwa nami hadi mwisho wa kipindi hiki. Tumo katika siku za mwanzoni mwa mwezi wa Muharram ambao ni mwezi wa kwanza wa mwaka wa Hijria. Katika zama za utawala wa Khalifa Umar bin Khattab Waislamu na kwa pendekezo lililotolewa na Imam Ali bin Abi Twalib (as), walijaalia hijra na kuhama kwa Mtume Muhammad (saw) kutoka Makka kwenda Madina kuwa ndio mwanzo wa kalenda ya Kiislamu. Baadaye mwezi wa Muharram ulichaguliwa kuwa mwezi wa kwanza wa mwaka wa Kiislamu kutokana na sifa zake za kipekee. Kwa Waislamu wengi duniani hususan Waislamu wa madhehebu ya Shia, kuanza kwa mwaka mpya wa Hijria na mwezi wa Muharram hukumbusha harakati itakayodumu milele ya Imam Hussein bin Ali (as). Katika historia ya Uislamu mwezi wa Muharram huambatana na tukio la Ashuraa yaani tarehe 10 mwezi huu; tukio ambalo licha ya kupita karne kadhaa sasa tangu litukie, bado linaangaza na kuwamulikia njia wapigania haki, ukweli na uadilifu. Sababu ya mwezi wa kwanza wa mwaka wa Hijria Qamaria kupewa jina la Muharram ni kwamba, katika zama za ujahilia ilikuwa haramu na marufuku kupigana vita katika mwezi huu. Kwa utaratibu kwamba, watu walikuwa wakisimamisha na kuacha kupigani vita katika mwezi wa Muharram na amani na usalama ulitawala katika maeneo yote. Baadhi ya wafasiri wa Qurani Tukufu wanasema kuwa, suna na ada ya kukataza vita katika miezi minne ukiwemo huu wa Muharram, ilianza katika zama za Nabii Ibrahim (as). Suna na kanuni hiyo iliendelezwa katika zama za ujahilia na ikadumishwa na kuungwa mkono na Uislamu.
 11:31 - 10/09/2018 - Comments : 0More >>
Ujumbe wa AYATULLAH KHAMENEI kwa mahujaji
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema katika ujumbe wake uliosomwa leo kwa Mahujaji wa Nyumba ya Mwenyezi Mungu kwamba sera za Marekani ni kuchochea vita baina ya Waislamu na akasisitiza kwamba: inapasa kuzizima sera hizo za kishetani kwa umakini na kuwa macho na kwamba Hija na kujibari na washirikina vinawezesha kupatikana umakini huo. Vilevile amewataka Mahujaji kuthamini taufiki ya kuwa katika ugeni wa Allah na kuitumia kwa ajili ya kujisafisha na kupata masurufu kwa ajili ya muda uliobakia katika umri wao. Matini kamili ya ujumbe wa Ayatullah Ali Khamenei ni hii ifuatayo: Hamdu zote zinamstahikia Allah na sala na salamu zimshukie Mtume wake al Mustafa na Aali zake watoharifu, na maswahaba zake wema. Mwenyezi Mungu SW anasema: Na watangazie watu Hija; watakujia kwa miguu na juu ya kila ngamia aliyekonda, wakija kutoka katika kila njia ya mbali. Ili washuhudie manufaa yao na walitaje jina la Mwenyezi Mungu katika siku maalumu…. Tangu karne zilizopita na vipindi mbalimbali, wito huo wa mbinguni ungali unaziita nyoyo na kuwataka wanadamu wakusanyike pamoja katika duara la Tauhidi na kumpwekesha Mwenyezi Mungu. Wanadamu wote wanalengwa na wito huu na wanajifaharisha nao, japokuwa masikio yao hayausikii na nyoyo zilizogubikwa na pazia la mgafala na ujahili zinashindwa kuupokea, na japokuwa wako watu ambao hawana ustahiki wa kuingia katika ugeni huo wa kimataifa na wa kudumu au hawakupata taufiki ya kuwa katika ugeni huo kwa sababu moja au nyingine. Nyinyi, mahujaji, mumefanikiwa kupata hiba hiyo na kuingia katika ugeni wa Mwenyezi Mungu. Arafa, Mashar, Mina, Safa, Marwa, Masjidul Haram na Masjidunnabi maeneo haya yote ya ibada ya Hija ni sehemu ya mnyororo wa masuala ya kiroho na ngazi ya kukwea katika masuala ya kimaanawi wakati wa Hija; hivyo mnapaswa kuthamini taufiki hiyo na kuitumia kwa ajili ya kujisafisha na kupata masurufu kwa ajili ya muda uliobakia katika umri wenu.
 13:49 - 20/08/2018 - Comments : 0More >>
Utawala wa Kizayuni wa Israel utaangamizwa kwa hima ya Waislamu
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei mapema leo amehutubia hadhara ya Baraza la Idi iliyohudhuriwa na maafisa wa serikali, makamanda wa jeshi, mabalozi wa nchi za Kiislamu na wananchi wa matabaka mbalimbali na kusema kuwa, sababu muhimu zaidi za kupelekea kuheshimiwa jamii za Kiislamu duniani ni umoja na kutatua hitilafu zilizopo. Ayatullah Khamenei amesema kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel ndiyo sababu kuu ya hitilafu zilizopo katika eneo la Mashariki na Kati na kati ya nchi za Waislamu na kuongeza kuwa: "Tatizo la utawala wa Kizayuni ni kutokuwa kwake halali na ni utawala ulioanzishwa kwa misingi batili na isiyo sahihi; hivyo kwa taufiki yake Mwenyezi Mungu na hima ya mataifa ya Waislamu, utawala huo utaangamizwa na kutoweka kabisa."
 12:48 - 15/08/2018 - Comments : 0More >>
Maadhimisho ya Kifo cha Imam Khomeini (RA)
Siku ya Jumapili ya tarehe 3 mwezi wa sita mwaka 2012 kituo cha utamaduni cha Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kiliandaa semina ya kumbukumbu ya Muasisi wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
 17:03 - 05/06/2012 - Comments : 0More >>
kumbukizi ya Mazazi ya Imam Mahd (ATS) Jijini Dar es Salaam - Tanzania
Maadhimisho ya kumbukizi ya Kuzaliwa Imam Mahdi ATFS ambayo yalifanyika katika ukumbi wa chuo cha kimataifa ambacho kinajulikna kama Jamiat Mustafa ambaho kipo jijini Dar es Salaam Tanzania. kumbukizi hii ilianza kwa kisomo ha Qur an tukufu ambayo ilifuatiwa na hotuba ya mapokezi ambayo ilitolewa kwa niaba ya chuo cha Jamia na Seyyid Arifu naqawi ambayo kwanza alinza kwa kuwashukuru wahudhiriaji wa Mahfali hayo na kuwaambia wajihisi kama wako nyumbani
 10:50 - 4/05/2018 - Comments : 0More >>
Kumbukumbu ya 33 ya Ushindi ya Mapinduzi ya Iran
Februari 11 ni siku ya ushindi wa ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu na ni siku ya kitaifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Mapinduzi haya kihistoria katika taifa la Iran linalojidhihirisha kama Mapinduzi ya Kiislamu, vuguvugu lililoashiria utashi wa taifa wa kuweka mamlaka yake na kuamua njia yake. Ushindi wa mapinduzi matukufu ya Kiislamu mnamo februari 11, 1979, ulioletwa na uongozi wa Imam Khomeini (Allah amlipe pepo), na uliokuwa na malengo mapana yaliyosheheni misingi ya haki za kibinadamu pamoja na maadili ya Kiislamu, ni mafanikio makubwa katika mchakato wa mapinduzi, ambayo, kwa hakika yalianza mwaka 1963...
 10:18 - 10/02/2012 - Comments : 0More >>
Salam za Mapinduzi ya Kiislamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema februar 11 ni siku muhimu ya maadhimisho ya mapinduzi ya Kiislamu ya Iran hivyo anahamasisha Waislamu kuadhimisha siku hiyo Dk. Bagheri alisema hayo Dar es salam jana alipokuwa anazungumza na waandihsi wa habari kuhusiana na maadhimisho hayo. Ni muhimu kuwakumbusha kuwa Mapinduzi ya Kiislamu yanaendeleza shughuli zake katika mazingira ambayo nguvu za pamoja zinajaribu kushindana na Mapinduzi hayo na kutumia mbinu mbalimbali. februari 11 kila mwaka ni kumbukumbu za ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran ambazo zinafanyika kila mwaka , ambao ushindi huo ulipatikana mwaka 1979 chini ya uongozi wa Imam Khomeni (ra) mwasisi mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran yalifanikiwa kuupindua utawala hasimu na wakidikteta wa Pahlavi Shah alisema,
 10:59 - 8/02/2018 - Comments : 0More >>
Kongamano la Amani Dar
Kongamano la wafuasi wa dini mbalimbali kuishi kwa masikilizano na kuhus mahusiano na mashirikiano ya dini mbali katika kukabilia na wahafidhina kwa watu wa dini limefanyika katika Kituo cha Utamadni cha Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Dar es Salaam nchini Tanzania. Kongamano hilo ambalo lilifanyika tarehe 14- 11- 2017 limeandaliwa kwa ushirikiano wa Kituo cha Kiutamaduni cha Iran nchini Tanzania na Baraza la Dini kwa ajili ya Amani . Akihutubia katika kongamano hilo, Rose Muzala, Mkuu wa Kitivo cha Sayansi za Jamii cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amesema, dini bila ya akili na mantiki ina madhara, na akili tupu bila ya dini haina ufanisi. Aidha ametoa shukurani kwa kituo cha Kiutamaduni cha Iran nchini Tanzania. Mussa Farhang, balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania ambaye alikuwa mzungumzaji mwengine katika kongamano hilo, amesema kuishi kwa masikilizano wafuasi wa dini mbalimbali katika Jamhuri ya Kiislamu kuna chimbuko la kihistoria; na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umejumuisha pamoja dini na akili. Mbali na kupongeza hali ya kuishi kwa masikilizano iliyopo baina wa waumini wa dini mbalimbali nchini Tanzania, Farhang ameongeza kuwa hitilafu za kidini ni jambo la kawaida, lakini inachopasa kufanya ni kutilia mkazo nukta za pamoja badala ya hitilafu. Mjumuiko wa viongozi wa Waislamu na Wakristo Tanzania Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania amesisitiza kuwa wanaofanya jinai kwa jina la dini ni watu wasio na akili timamu; na njia pekee ya kuwezesha wafuasi wa dini tofauti kuishi kwa masikilizano ni kujiepusha na vitendo vya machafuko na ukatili. Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Zanzibar, Rashid Ali Juma, yeye ameashiria historia ya pamoja ya Iran na Tanzania na kusisitiza azma ya Zanzibar ya kuimarisha uhusiano baina ya pande mbili. Kongamano hilo limehudhuriwa pia na wahadhiri pamoja na wanachuo wa nchini Tanzania…/
 12:40 - 22/11/2017 - Comments : 0More >>
Ujumbe wa Hijja Mwaka 2017
Ninamshukuru Mwenyezi Mungu Mkubwa ambaye mwaka huu pia amewapa waumini kutoka maeneo mbalimbali ya dunia, saada na ufanisi wa kutekeleza ibada ya Hija ili wafaidike na chemchemi hiyo yenye maji matamu na yanayotiririka, na kufanya itikafu na kuwa kandokando ya Nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu katika nyakati za ibada, khushui, dhikri na kujikurubisha kwake katika siku na nyusiku zinazohesabika kuwa ni fursa adhimu na yenye baraka ambazo saa zake ni mithili ya mada inayofanya muujiza unaoweza kubadilisha nyoyo na kutakasa na kuzipamba nafsi na roho zao. Hija ni ibada yenye siri nyingi, na nyumba tukufu (ya al Kaaba)
 11:23 - 05/09/2017 - Comments : 0More >>
Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete azindua rasmi tamasha la ZIFF 2017, Atunukiwa tuzo ya mtu aliyetukuka
Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete azindua rasmi tamasha la ZIFF 2017, Atunukiwa tuzo ya mtu aliyetukuka Rais Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Jumamosi usiku wa Julai 8,2017, amezindua rasmi tamasha la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF), tukio lililofanyika Ngome Kongwe, Mjini Unguja-Zanzibar. Katika tukio hilo, Dkt. Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo la 20, tokea kuanzishwa kwake miaka 20, iliyopita. Ambapo uongozi wa ZIFF waliweza kusoma wasifu wa Rais huyo Mstaafu kwa namna alivyoweza kusaidia mchango mkubwa kuendeleza tasnia ya filamu
 12:49 - 12/07/2017 - Comments : 0More >>

matukio ya siku tasua na ashuraa mwaka 2018
Masiku ya mwanzo ya mwezi Muharram
Ujumbe wa AYATULLAH KHAMENEI kwa mahujaji
Utawala wa Kizayuni wa Israel utaangamizwa kwa hima ya Waislamu
Utawala wa Kizayuni wa Israel utaangamizwa kwa hima ya Waislamu
kumbukizi ya Mazazi ya Imam Mahd (ATS) Jijini Dar es Salaam - Tanzania
Salam za Mapinduzi ya Kiislamu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
Kongamano la Amani Dar
Ujumbe wa Hijja Mwaka 2017
Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete azindua rasmi tamasha la ZIFF 2017, Atunukiwa tuzo ya mtu aliyetukuka
SHEIKH JALALA AONGEA NA (UN) KUHUSU AMANI YA PALESTINA
Semina"Mchango wa Imam Khomein (r.a) Ulimwenguni yafanyika Dar es salaam
uchaguzi wa Iran
Kuzaliwa kwa Imam Mahdi
sherehe za Nooroz na mazazi ya Bi fatma AS
Search
Advance Search Web Search
banners
Kiongozi Muadhama

Imam

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

presstv

Radio Tehran

Al-hikma

Iqna

Irna

Mubaligh

Jamiatul Mustafa (SAWW

Islamica

Rayhanee
vote
Disable
UsersStats
Visitorsofpage: 11858
Visitorsofday : 27
Visitorsofpage : 62942
Onlinevisitors : 1
PageLoad : 1.3437

Home|Habari|Kutuhusu|Programu|Historia ya mahusiano ya kitamaduni|Mahusiano ya jumuia zingine |Machapisho|Ushirikiano na Maktaba zingine|Matukio ya Kiutamaduni|Ofisi zingine za Iran