Thursday, January 18, 2018 Home|Habari|فارسي|Kiswahili
 

Nyumbani|Uislamu|Lugha ya Kifursi|FAQ|Wasiliana nasi|Links|Sitemap
Title
iran
.
Login
Username :   
Password :   
[Signup]
NewsletterSignup
Name :   
E-mail :   

Kongamano la Amani Dar


Kongamano la wafuasi wa dini mbalimbali kuishi kwa masikilizano na kuhus mahusiano na mashirikiano ya dini mbali katika kukabilia na wahafidhina kwa watu wa dini limefanyika katika Kituo cha Utamadni cha Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Dar es Salaam nchini Tanzania. Kongamano hilo ambalo lilifanyika tarehe 14- 11- 2017 limeandaliwa kwa ushirikiano wa Kituo cha Kiutamaduni cha Iran nchini Tanzania na Baraza la Dini kwa ajili ya Amani . Akihutubia katika kongamano hilo, Rose Muzala, Mkuu wa Kitivo cha Sayansi za Jamii cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, amesema, dini bila ya akili na mantiki ina madhara, na akili tupu bila ya dini haina ufanisi. Aidha ametoa shukurani kwa kituo cha Kiutamaduni cha Iran nchini Tanzania. Mussa Farhang, balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania ambaye alikuwa mzungumzaji mwengine katika kongamano hilo, amesema kuishi kwa masikilizano wafuasi wa dini mbalimbali katika Jamhuri ya Kiislamu kuna chimbuko la kihistoria; na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran umejumuisha pamoja dini na akili. Mbali na kupongeza hali ya kuishi kwa masikilizano iliyopo baina wa waumini wa dini mbalimbali nchini Tanzania, Farhang ameongeza kuwa hitilafu za kidini ni jambo la kawaida, lakini inachopasa kufanya ni kutilia mkazo nukta za pamoja badala ya hitilafu. Mjumuiko wa viongozi wa Waislamu na Wakristo Tanzania Balozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nchini Tanzania amesisitiza kuwa wanaofanya jinai kwa jina la dini ni watu wasio na akili timamu; na njia pekee ya kuwezesha wafuasi wa dini tofauti kuishi kwa masikilizano ni kujiepusha na vitendo vya machafuko na ukatili. Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Zanzibar, Rashid Ali Juma, yeye ameashiria historia ya pamoja ya Iran na Tanzania na kusisitiza azma ya Zanzibar ya kuimarisha uhusiano baina ya pande mbili. Kongamano hilo limehudhuriwa pia na wahadhiri pamoja na wanachuo wa nchini Tanzania…/

 12:40 - 22/11/2017More >>

Ujumbe wa Hijja Mwaka 2017
Ninamshukuru Mwenyezi Mungu Mkubwa ambaye mwaka huu pia amewapa waumini kutoka maeneo mbalimbali ya dunia, saada na ufanisi wa kutekeleza ibada ya Hija ili wafaidike na chemchemi hiyo yenye maji matamu na yanayotiririka, na kufanya itikafu na kuwa kandokando ya Nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu katika nyakati za ibada, khushui, dhikri na kujikurubisha kwake katika siku na nyusiku zinazohesabika kuwa ni fursa adhimu na yenye baraka ambazo saa zake ni mithili ya mada inayofanya muujiza unaoweza kubadilisha nyoyo na kutakasa na kuzipamba nafsi na roho zao. Hija ni ibada yenye siri nyingi, na nyumba tukufu (ya al Kaaba)
 11:23 - 05/09/2017 - Comments : 0More >>
Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete azindua rasmi tamasha la ZIFF 2017, Atunukiwa tuzo ya mtu aliyetukuka
Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete azindua rasmi tamasha la ZIFF 2017, Atunukiwa tuzo ya mtu aliyetukuka Rais Mstaafu wa awamu ya nne katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Jumamosi usiku wa Julai 8,2017, amezindua rasmi tamasha la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF), tukio lililofanyika Ngome Kongwe, Mjini Unguja-Zanzibar. Katika tukio hilo, Dkt. Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi katika tamasha hilo la 20, tokea kuanzishwa kwake miaka 20, iliyopita. Ambapo uongozi wa ZIFF waliweza kusoma wasifu wa Rais huyo Mstaafu kwa namna alivyoweza kusaidia mchango mkubwa kuendeleza tasnia ya filamu
 12:49 - 12/07/2017 - Comments : 0More >>
Habari 24 blog
SHEIKH JALALA AONGEA NA (UN) KUHUSU AMANI YA PALESTINA
Kiongozi wa Dhehebu la SHIA Ithna Sheria Sheikh Hemed Jalala ameitaka jumuiya umoja wa mataifa (UN) kuiangalia kwa jicho la karibu nchi ya Palestina ili amani iwezekurejea kama ilivyo kwa nchi ya Tanzania. Sheikh Hemed Jalala ameyasema hayo leo katika semina ya Quds ya kuwakumbuka waislamu na wote wanaoishi kwa kupata taabu nchini Palestina, ambapo ameeleza kuwa watanzania inabidi waoneshwe kusikitishwa na kupinga vikali dhidi ya mambo yanayoendelea nchini humo kwani kinamama wanakosa huduma za afya jambo linalopelekea kujifungua kwa taabu. Sheikh Jalala amefafanua kuwa hali ya nchi hiyo siyo nzuri kwani vijana wa kiislamu wamekuwa wakizuiwa kuswali kwenye
 11:10 - 19/06/2017 - Comments : 0More >>
Maadhimisho ya Kifo cha Imam Khomeini (RA)
Siku ya Jumapili ya tarehe 3 mwezi wa sita mwaka 2012 kituo cha utamaduni cha Ubalozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kiliandaa semina ya kumbukumbu ya Muasisi wa mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.
 17:03 - 05/06/2012 - Comments : 0More >>
Semina"Mchango wa Imam Khomein (r.a) Ulimwenguni yafanyika Dar es salaam
Balozi wa Iran Nchini Tanzania Mhe.Mussa Farahang akitoa mada katika Semina ya Mchango wa Imam Khomein (r.a) Ulimwenguni, Masjid Ghadir, Kigogo Post Dar es alaam.
 10:20 - 6/06/2017 - Comments : 0More >>
Kumbukumbu ya 33 ya Ushindi ya Mapinduzi ya Iran
Februari 11 ni siku ya ushindi wa ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu na ni siku ya kitaifa ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Mapinduzi haya kihistoria katika taifa la Iran linalojidhihirisha kama Mapinduzi ya Kiislamu, vuguvugu lililoashiria utashi wa taifa wa kuweka mamlaka yake na kuamua njia yake. Ushindi wa mapinduzi matukufu ya Kiislamu mnamo februari 11, 1979, ulioletwa na uongozi wa Imam Khomeini (Allah amlipe pepo), na uliokuwa na malengo mapana yaliyosheheni misingi ya haki za kibinadamu pamoja na maadili ya Kiislamu, ni mafanikio makubwa katika mchakato wa mapinduzi, ambayo, kwa hakika yalianza mwaka 1963...
 10:18 - 10/02/2012 - Comments : 0More >>
uchaguzi wa Iran
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza juu ya udharura wa wananchi wa Iran kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa leo. Rouhani asema mahudhurio makubwa yataimarisha izza, usalama wa Iran May 19, 2017 07:45 Rais Hassan Rouhani wa Iran ametoa wito kwa wananchi kushiriki kwa wingi katika uchaguzi wa rais unaofanyika hii leo hapa nchini akisisitiza kuwa, mahudhurio makubwa katika zoezi hilo yataimarisha izza na usalama wa Jamhuri ya Kiislamu. Wananchi wa Iran leo wanashiriki katika uchaguzi wa Urais May 19, 2017 04:22 Wananchi wa Iran waliotimiza masharti ya kupiga kura leo wanaelekea katika masanduku ya kupigia kura kwa ajili ya kumchagua Rais wa nchi. Uchaguzi wa Rais wa Iran kufanyika katika nchi 102 duniani May 18, 2017 15:26 Mkuu wa kamati ya kusimamia uchaguzi wa 12 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran nje ya nchi amesema kuwa, uchaguzi huo utafanyika katika nchi 102
 12:57 - 19/05/2017 - Comments : 0More >>
Kuzaliwa kwa Imam Mahdi
Imam Mahdi AS alizaliwa siku ya Ijumaa ya mwezi 15 Shaabani mwaka 255 Hijria mjini Samarra Iraq na baba yake akiwa ni Imam Hassan Askari AS. Imam Mahdi ni mjukumuu wa Bwana Mtume Muhammad SAW kupitia kizazi cha masharifu na masayyid cha binti mtukufu wa Bwana Mtume Muhammad yaani Bibi Fatimatu Zahra SA. Mama yake alikuwa Bibi mwenye heshima kubwa aliyejulikana na jina la Nargis. Imam Mahdi AS ni nyota ya 12 ya Maimamu wa Ahlul Bayt AS waliousiwa na Bwana Mtume Muhammad SAW. Ni vyema kusema pia hapa kwamba masuala mengi yanayohusiana na Imam Mahdi AS ni mambo ya ajabu ikiwa ni pamoja na namna ya kuzaliwa kwake kiasi kwamba hata athari za ujauzito wa mama yake haukuwa wa kawaida na wala hazikuonekana hadharani athari za ujauzito wake. Siri ya jambo hilo nayo iko wazi kwamba watawala wa wakati huo wa Bani Abbas walikuwa wamesoma hadhithi kutoka kwa Bwana Mtume Muhammad SAW na Maimamu watoharifu kuwa Imam Hassan Askari AS angelizaa mtoto ambaye angelikuja kuvunja tawala zote za kidhalimu na kidikteta, na kuangamiza kambi zote za upotofu na ufisadi na hatimaye kuijaza ardhi uadilifu na haki. Hivyo majasusi wa watawala wa Bani Abbas wakawa wanafuatilia kwa karibu sana maisha ya watu wa nyumbani kwa Imam Askari AS kwa nia ya kuzuia kuzaliwa mtoto huyo na kama wakiona amezaliwa, wamuue mara moja. Hivyo namna ya kuchukuliwa mimba, kuzaliwa na maisha ya baadaye ya Imam Mahdi AS hayakuwa na hali za kawaida. Kwa hakika Mwenyezi Mungu alitaka Imam Mahdi azaliwe katika mazingira yanayofanana na yale ya Nabii Musa AS. Maadui wa Imam Mahdi walitumia mbinu ile ile iliyotumiwa na majasusi wa Firauni waliofanya ujasusi na njama kubwa za kutaka kumuua Nabii Musa AS akiwa bado mdogo. Hata hivyo Mwenyezi Mungu kwa uwezo Wake alimuokoa Mtume Wake huyo. Watawala wa Bani Abbas nao walitaka kuzuia kuzaliwa Imam Mahdi AS na kumuua akiwa bado mchanga. Waliwawekea ulinzi mkali - mbali na majasusi wengi - watu wa nyumba ya Imam Askari AS, lakini Mwenyezi Mungu amemlinda Imam Mahdi AS hadi leo hii.
 16:38 - 11/05/2017 - Comments : 0More >>
sherehe za Nooroz na mazazi ya Bi fatma AS
Siku ya tarehe 21 mwezi machi usiku wa saa mbili mpaka saa 5 kasoro kulifanyika sherehe tatu kwa wakati mmoja. Sherehe ya kwanza ilikuwa ufunguzi wa ukumbi mpya ambao ulijulikana kama ukumbi wa shahidi Ansar, sherehe ya pili ilijukana kama sherehe ya Noroz na sherehe ya tatu ilijukana kama sherehe ya kukumbuka mazazi ya motto wa Mtume Muhamad SAWW. Bibi Fatmah zahraa AS. Sherehe ilikuwa kubwa na kufana sana maana muitikio ulikuwa mkubwa sana, ilikadiriwa kufika watu takriban mia tano, wakiongozwa na Balozi wa Jamhiri ya Kiislamu ya Iran BW. Musa Farhang, na Sheikh mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Alhadi Musa Salim. Sherehe ilifunguliwa kwa kisomo cha Qur an tukufu iliyosomwa na Afisa kutoka ubalozi wa jamhuri ya kiislamu ya Iran Bwana Answari, Ikifuatiwa na utambulisho wa wageni ambao ulifanywa na mwenyeji wa shughuli Bwana Ali Bagher ambaye ni mkurugenzi mkuu wa Kituo cha Utamaduni cha Ubalioz wa Iran hapa Tanzania.
 11:17 - 6/04/2017 - Comments : 0More >>
mwezi wa rajab
Mwezi wa Rajab umeanza, ni miongoni mwa miezi mitatu ambayo imejaa baraka, nayo ni (Rajab, Shabani na Ramadhani) ambayo katika kila miezi mitatu watu hupata kufadika na baraka za miezi hii mitukufu, katika miezi hii hata katika zama za ujahili ilikuwa ikiehshimiwa sana kiasi ambacho ilikuwa ni haramu kumwaga damu. Kiasi ambacho waarabu walikuwa wakiweka silaha zao chini kwa kipindi hiki chote cha mwezi wa rajab kwa maaana vita ilikuwa ni marufuku. Mtume mtukufu SAWW pia katika kusisitiza utukufu wa mwezi huu amesema: hakika mwezi wa rajab ni mwezi wa ASWAM na imeitwa aswam kwa sababu hakuna mwezi unaoukaribia kwa utukufu kwa mwenyezi mungu tabaraka wataala)
 12:18 - 31/03/2017 - Comments : 0More >>

Kongamano la Amani Dar
Ujumbe wa Hijja Mwaka 2017
Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete azindua rasmi tamasha la ZIFF 2017, Atunukiwa tuzo ya mtu aliyetukuka
SHEIKH JALALA AONGEA NA (UN) KUHUSU AMANI YA PALESTINA
Semina"Mchango wa Imam Khomein (r.a) Ulimwenguni yafanyika Dar es salaam
uchaguzi wa Iran
Kuzaliwa kwa Imam Mahdi
sherehe za Nooroz na mazazi ya Bi fatma AS
mwezi wa rajab
Kumbukumbu ya Kifo cha Bibi Fatima a.s
Mkutano wa Kuikomboa Palestina
Iran na Tanzania katika wiki ya Utaduni
Mkutano wa kidini chuo kikuu cha dar es salaam
Ujumbe wa Kiongozi wa Kiislamu kwa Jumuiya ya Wanachuo Ulaya
Rais wa Russia atuma salamu za rambirambi kwa kifo cha Ayatullah Rafsanjani
Search
Advance Search Web Search
banners
Kiongozi Muadhama

Imam

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

presstv

Radio Tehran

Al-hikma

Iqna

Irna

Mubaligh

Jamiatul Mustafa (SAWW

Islamica

Rayhanee
vote
Disable
UsersStats
Visitorsofpage: 11053
Visitorsofday : 30
Visitorsofpage : 50951
Onlinevisitors : 1
PageLoad : 1.6719

Home|Habari|Kutuhusu|Programu|Historia ya mahusiano ya kitamaduni|Mahusiano ya jumuia zingine |Machapisho|Ushirikiano na Maktaba zingine|Matukio ya Kiutamaduni|Ofisi zingine za Iran